Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AWAFANYIA PARTY KUWAKARIBISHA WAKE WA MABALOZI KWA MWAKA MPYA 2013, IKULU DAR

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla  maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013,

Baadhi ya wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zaoTnzania wakisubiri kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya2013 katika viwanja vya Ikulu jjijini Dsm Jan 15,2013 iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani).

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akibadilishana mawazo na baadhi ya wenza wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wakati wa sherehe ya hafla ya kuukaribisha mwaka 2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam,jan 15,2013.

Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) akibadilishana mawazo na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) katika hafla maalumu ya mwaka mpya 2013 kwaajili ya wake wa Mabalozi iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(hayupo pichani) kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan,15,2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla  maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013,

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto)akisalimiana na Mdau Fauzia Aboud katika hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar e Salaam Jan15,2013,

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu Mama Sitti Mwinyi(kushoto) katika hafla mwaka mpya2013 ya kuwakaribisha (SPOUSE) wake wa Mabalozi nchini  Jan 15,2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(mwenye kilemba)akipongezana na Consulate wa  Jamhuri ya Poland Bibi  Grazyna Tairo kwenye hafla ya kuwakaribisha wenza wa Mabalozi nchini jan 15,2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akipongezana na Kiongozi wa wenza wa Mabalozi nchini Celine Khalfan Juma Mpango katika hafla ya kusherehekea na kukaribisha mwaka mpya 2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan 15,2013. (Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO