Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MASHABIKI WA SOKA JIJINI ARUSHA WAFURAHIA UFUNGUZI WA AFCON 2013 NA DStv NDANI YA BABYLON CLUB

Mashabiki wa soka wa jiji la Arusha, wamepata fursa ya aina yake ya kushuhudia uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka huu wa 2013, katika kiota maarufu cha Babylon Club kilichopo katika eneo la Metropole sambamba na wadau kutoka DStv ambao ndio waonyeshaji wa uhakika wa mashindano haya kupitia Channels zao za SuperSport. Hizi hapa ni picha na maelezo kutoka katika tukio hilo la uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yataendelea mpaka tarehe 10 Februari.

Wadau wa Babylon Club,Arusha katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa ulioletwa na DStv kupitia channels zao za Super Sports. Experience The Spirit Of Africa…

Ndani ya Babylon Club, kama unavyoona kuna screens kubwa na nyingi…Zote zimeunganishwa na DStv

Meneja Masoko wa DStv,Furaha Samalu(kulia) akiwa na mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo, wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ndani ya Babylon Club. DStv wanaonyeshaji mashindano hayo Live na katika HD kupitia Channels zao za SuperSport.

Sales Coordinator wa DStv Kanda ya Kaskazini, Christopher Mbanjo, akiteta jambo la Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo(www.millardayo.com) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ndani ya Babylon Club,Arusha.

Macho yote kwenye screens mbalimbali zilizotapakaa ndani ya Babylon Club

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria kutizama mechi za ufunguzi za AFCON 2013 wakishuhudia mchezo wa kwanza wa mashindano hayo baina ya South Africa na Cape Verde. Timu hizo zilikwenda sare ya kutofungana.

Panapo watu haliharibiki jambo.Lakini…endapo lingeharibika basi hawa jamaa walikuwa tayari kabisa kurekebisha au kutatua.Ndani ya Babylon Club,Arusha.

Meneja Masoko wa DStv,Furaha Samalu, akiwa na mdau wa soka ambaye alikiri kwamba yeye huwaamini DStv pekee linapokuja suala la burudani kupitia mchezo wa soka.

Soccer and Dance….Experience The Spirit Of Africa. Picha na BongoCelebrity.Com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO