Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA YAZIDI KUIMEGA CCM ARUSHA, VIONGOZI WENGINE WAHAMIA CHADEMA

MJUMBE  wa halmashauri Kuu Wilaya kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Kata ya Unga Ltd, Jijini Arusha  na Katibu Mwenezi Kata ya Unga ltd , na mjumbe wa vijana taifa, Musa Daudi Lungo na mkewe wamekihama chama hicho na kujiunga na  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lungo  alitangaza rasmi kuhamia chama hicho jana katika ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha zilizopo eneo la Ngarenaro mjini hapa  huku akifuatana na marafiki zake pamoja na  mkewe .

Akitangaza rasmi kujiunga na chama hicho , Lungu alisema kuwa , amechoshwa na chama cha mafisadi kisichokuwa na uchungu na wananchi  wake ambapo amedumu katika chama hicho kwa muda mrefu sana bila kuona mafanikio yoyote zaidi ya kupoteza muda wake.

Alisema kuwa, chama cha mapinduzi kimekuwa ni chama cha uongo na uongo ndio sehemu ya maisha yao , hivyo amekuwa akibakwa mawazo yake kila alipokuwa ndani ya chama hicho , hivyo kuendelea kuvumilia kubaki ndani ya chama hicho ni kuendelea kupoteza muda na kujinyima haki yake ya msingi .

‘Mimi nimefikia uamuzi  wa kujiunga na chama hiki na najua wengi sana watanifuata kuniunga mkono kwani kila mmoja amechoka na siasa za uongo ndani ya  CCM na zisizojali maslahi ya wananchi kwa ujumla na nawashauri watanzania wenzangu kuwa watoke gizani wahamie nuruni kwani huku kuna amani  na ni mahali sahihi pa kutimiza malengo’alisema Lungo.

Aliongeza zaidi kuwa, kujiunga na chama hicho sasa hivi ni muda muafaka ili aweze kutimiza malengo yake ya kuwatumikia wananchi na kutetea haki zao kwani chadema ndipo mahali sahihi pa kukimbilia na penye matumaini kwa kila mmoja.

‘Mimi nimedumu ndani ya CCM kwa muda mrefu sana lakini sijaona mafanikio yoyote zaidi ya kuendelea kuwanyanyasa wananchi na kuendelea kuteseka ndani ya chama ni aibu kubwa sana hadi sasa hivi kwenye kata kubwa ya unga ltd inayozungukwa na viwanda kila mahali haina shule ya sekondari huo ni udhalilishaji mkubwa wakati chama kina hela nyingi sana za kuweza kufanya maendeleo badala yake zinaishia kwenye maswali yasiyo ya msingi’.alisema Lungu.

Naye Katibu wa chadema wilaya ya Arusha, Martin Sarungi akimkabithi kadi ya chadema mwanachama huyo alisema kuwa, kitendo cha kujiunga na chadema ni  kuonyesha moyo wa kujali na kuchoshwa na matendo maovu waliyokuwa wakifanyiwa wakiwa chama cha mapinduzi.

Alisema kuwa, wanachama wengi wa CCM  wanajiunga na chadema  kutokana na kupendezewa na sera ambayo ina mwamko mkubwa  wa kuleta mabadiliko kwa wananchi wake huku ikijali kutetea haki za wananchi zaidi na kuwakomboa kutoka katika manyanyaso mbalimbali.

‘Sisi tunaendelea kuwakaribisha wanachama wazidi kujiunga na chama chetu zaidi na sisi tutawapokea wote haijalishi kuwa wanatokea chama gani ,kwani hadi kufikia hatua ya kujiunga na chadema ina maana wamependezewa na sera na mwenendo wa chama hiki’alisema Sarungi.

CHANZO: JAMII BLOG (PAMELA MOLLEL)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO