Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MAPOKEZI YA DR SLAA KWA UFUNGUZI WA MATAWI, OFISI NA MKUTANO WA HADHARA MJINI MOSHI JANA

M4C Moshi5 Wananchi wa mtaa wa kibo wakimpokea katibu mkuu wa chama Dr Slaa katika ufunguzi wa ofisi ya mtaa ya chamaDr Slaa akipokelewa na wananchi wa Mtaa wa Kibo Mjini Moshi ambapo alifungua matawi na odisi ya Kata ambapo baadae alifanya mkutano mkubwa katika viwanja vya Njoro Mjini Moshi. Leo atakuwa na mkutano mwingine Mkubwa maeneo ya Same sambamba na kufungua matawi na ofisi za Kata Hedaru na Makanya.

Picha tatu za mwisho kwa hisani ya Michuzi Blog

*****

Slaa atangaza 2013 mwaka mtakatifu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeufananisha mwaka huu kama mtakatifu, kwa wanachama wake kujiandaa na chaguzi za mwaka 2014 na 2015.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alipokuwa akizindua ofisi za kata na matawi maeneo tofauti ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Dk Slaa alisema mwaka huu ni mtakatifu kwa chama hicho, kwa sababu ni pekee uliobaki katika harakati za ukombozi wa Watanzania kabla hawajafikia mwaka 2014.

Aliwataka wanachama na viongozi wa Chadema kufanya kazi zenye kuleta tija kwa wananchi, ikiwamo kufungua ofisi kwa wingi, kuhamasisha wananchi kujiunga kwa wingi na chama hicho.

Alisema lengo ifikapo mwaka wa 2014 ambao ni wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka 2015 Uchaguzi Mkuu, kiweze kushika dola.

Dk Slaa ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya kuimarisha chama, kufanya mikutano ya hadahara, alisema licha ya ufunguzi wa ofisi hizo za kata, viongozi na wanachama wahakikishe zinafanya kazi ya kuhudumia wanachama na wananchi siyo kugeuzwa mazalio ya popo au vijiwe. Ili kufanikisha kazi za chama, Dk Slaa aliwataka viongozi hasa madiwani katika siku 365 za mwaka huu, kuhakikisha wanawafikia wananchi kwa njia mbalimbali na kuwaelezea sera za Chadema.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa aliwakingia kifua madiwani wa Manispaa ya Moshi kwa kueleza kuwa mara nyingi watu wengi wamejenga tabia ya kulaumu madiwani kila kitu kibaya.

Alisema diwani hashiki fedha, hatoi zabuni na kazi yake ni kuhamasisha maendeleo ya kata husika, ili kuhakikisha miradi iliyopangwa inatekelezwa.

Dk Slaa aliwataka madiwani wa Chadema nchini kuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo ya halmashauri zao.Alisema itakuwa rahisi kwa Chadema kupata ushindi na kumpatia ukombozi wa kweli mwananchi.
IMEANDIKWA NA GAZETI MWANANCHI

***********************

Dk Wilbrod Slaa akifafanua jambo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa moshi katika mkutano wa wazi uliofanyika viwanja vya Njoro mjini Moshi jana.

M4C MoshiWananchi wakigombania kununua kadi za uanachama wa chama hicho

M4C Moshi1Sehemu ya mahudhurio ya wananchi katika mkutano huo

Wananchi wakionesha ishara ya kujibu swali la Dr Slaa aliyewauliza wakazi hao wa  Moshi Mjini ni nani ambaye kwa muda ule alikuwa tayari kujiunga na CHADEMA.

M4C Moshi4

M4C Moshi2Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akihutubia

M4C Moshi3

Wakazi wa jimbo la Moshi Mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Njoro jana.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO