Jijini Arusha leo limefanyika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto inayoratibiwa na asasi za Evidence for Action(non governmental organisation) wakishirikiana na TRCS katika kuzindua kampeni ya Mama Ye! Zoezi hilo lilifanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mh Kasunga. “Changia Damu, Okoa Maisha ya Mama na Mtoto”Arusha. Jumla ya wachangiaji 1040 walijitolea damu.
Kaimu Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mh Karimu akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katiba bustani ya Makumbusho ya Azimio la Arusha.
Mshereheshaji wa tukio zima, Bw Keneth Simbaye akiwajibika jukwaani
Baadhi ya wananfunzi ambao wamekwishachangia damu wakiwa wamepumzishwa kivulini na wahudumu wa Mama Ye viwanjani hapo!
Wananfunzi ambao wako kwenye foleni ya kuchnagia damu
Mhudumu wa kampeni za Mama Ye! akiendelea na zoezi la kusaidia uchangiaji damu Jijini Arusha leo
Mhudumu wa Mama Ye! akimuandaa mwanafunzi kwa ajili ya uchangiaji damu
Mwanafunzi akipatiwa ushauri na kuchukuliwa maelezo ya kiafya kabla ya kuruhusiwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto
Mhudumu akimuelekeza mama huyu mahali pa kwenda kutoa damu kwa ajili ya uchangiaji damu kwa hiyari Jijini Arusha leo, zoezi lililofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha chini ya uratibu wa taasisi ya Evidence for Action naTRCS !
0 maoni:
Post a Comment