Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rais wa Misri atangaza hali ya hatari

Machafuko mjini Cairo wakati wa maadhimisho ya miaka miwili baada ya mapinduzi ya kiraia

Rais wa Misri Mohammed Morsi ametangaza hali ya tahadhari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia baada ya siku kadhaa za machafuko makali.

Kuanzia Jumatatu na kwa siku 30 zijazo watu hawatakubaliwa kutoka nje kati ya saa 21:00 na 06:00, alisema alipohutubia taifa.

"Huwa kwa kawaida napinga hali za tahadhari, lakini ilibidi niwalinde wananchi na kukomesha umwagikaji damu basi ikanabidi nifanye hivyo,” rais alisema.

Takriban watu 33 people walikufa mnamo wikiendi huko Port Said, ambapo uamuzi wa mahakama ulisababisha vurugu kuzuka.

Kutoridhika na uongozi wa Bwana Morsi's kulizua fujo kwingine nchini.

Katika mji mkuu wa Cairo, waadamanaji wailokuwa wanaipinga serikali walipambana na vikosi vya ulinzi karibu Uwanja wa Tahrir kwa siku ya nne mfululizo.

Upinzani

Upinzani unamlaumu Morsi kwa kutawala kimabavu na kuipa kipaumbele katiba mpya ambayo hailindi kikamilfu haki za kuabudu wala za maoni.

Serikali pia imelaumiwa kwa kutodhibiti hali ya uchumi, inayozidi kuzorota.

Bwana Morsi alisema kwamba angechukua hatua zaidi "kwa ajili ya Misri" na kwamba ilikuwa "wajibu wake" kama rais kufanya hivyo.

Vuru katika mji wa Portland

Aidha, aliwaalika viongozi wa kisiasa wakutane "katika majadiliano ya kitaifa " mnamo Jumatatu.

Ingawaje muungano mkubwa zaidi wa vyama pinzani nchini Misri, National Salvation Front, uliuunga mkono mualiko huo, ulilaumu sera za Morsi kwa kuzua vurugu.

Vurugu zilizuka Port Said baada ya mahakama kuwahukumu watu 21 kifo kwa kuhusika na fujo baada ya mechi ya kandanda Februari 2012.

Taarifa na BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO