Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DR SLAA KUWASHA MOTO SAME JANUARI 15, 2013

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr Wilbroad Slaa

***********

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Dr Wilbroad Slaa anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara Mjni Same siku ya Jumanne Januari 15, 2013.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mratibu Mkuu wa mkutano huo mkubwa, Bw Christopher Mbajo, Dr Slaa anatarajiwa pia kuzindua Ofisi ya CHADEMA Kata ya Hedaru na kufungua matawi ya chama hicho katika maeneo ya Hedaru, Makanya na Same.

Akifafanua zaidi, Bw Mbajo anaeleza kuwa maandalizi yote ya mkutano huo yanakwenda vizuri na kuwataka wananchi wali karibu na maeneo hayo kujitokeza kwa wingi siku hiyo kusikiliza kile ambacho Katibu Mkuu huyo atawaambia.

Kwa taarifa ambazo Blog hii imezipata, inaelezwa kuwa Dr Slaa atakuwa na Mkutano mwingine Mjini Moshi siku ya Jumatatu mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachoendelea Mjini humo.

Itakumbukwa kwamba, katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi Disemba 15-16 mwaka jana, chama hicho kiliazimia kwamba mwaka huu wa 2013 utakuwa ni mwaka wa kuunganisha nguvu ya umma kitaifa, kuishinikiza serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko juu ya kuundwa tume huru ya kimahakama, itakayochunguza ya mauaji mbalimbali ya utatanishi yaliyotokea nchini katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Mbali na kuunganisha nguvu ya umma, chama hicho pia kiliazimia kuitumia kambi rasmi ya upinzani bungeni kutumia njia za Kibunge kupitia hoja binafsi au muswada binafsi kuwasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya mpito kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi na marekebisho ya sheria zinazosimamia uchaguzi, yanafanyika kabla ya Katiba Mpya.

DSCN4778

Christopher Mbajo katika moja ya ziara zake kuimarisha chama (CHADEMA) Wilayani Same. Hapa ilikuwa ni mwezi Julai mwaka jana katika Kijiji cha Marwa-Ruvu Muungano Same, Kilimanjaro

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO