Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MTWARA UPDATES: Nyumba ya Mkuchika yachomwa moto - Newala, Gereza lavamiwa wafungulia wafungwa.

Taarifa za redio mbao ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Blog ya MTWARA KUMEKUCHA soma zaidi…

Updates

  • Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu.
  • Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.Maaskari na makachero wawasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
  • Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa. 
  • Kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
  • Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
  • Wakiwa katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi.
  • Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
  • Hali imeshakuwa mbaya Masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa mama Ana Abdala, hapa Mtwara  mjini maduka yote eneo la soko kuu na stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
  • Vurugu zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu zashamiri Mabomu Kibao..Hali ni tete

Askari auawa

Na taarifa zaidi kutoka Masasi zinaeleza kuwa askari wa upelelezi Masasi aliyejichanganya katika vurugu wananchi walimshitukia akiwapiga picha, akashambuliwa na kuuliwa. Askari huyo inaelezwa amekutwa na bastola mbili. Taarifa zaidi baada ya kuthibitishwa tutawaletea

Jengo la Mahakama ya Mwanzo likiendelea kuteketea, tukio la jana

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO