Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YABARIKI USITISHWAJI MRADI WA MJI WA MFANO ARUSHA KATIKA ENEO MAARUFU LA LAKILAKI

lakilaki.

Mradi wa lakilaki unavyoonekana katika picha

BARAZA la Madiwani wa Halmasauri ya wilaya ya Arusha, hatimaye  leo (jana) tarehe 5 Januari 2013 limeidhinisha kuliachia eneo la Lakilaki  lililopangwa kujengwa mji wa mfano wa Arusha(Arusha Safari Town)  na kukabidhi hati miliki ya ardhi hiyo, kwa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Taasisi za  umoja ya Mataifa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Maamuzi hayo, yalifikiwa leo katika kikao cha dharura ambacho, kilihudhuriwa na waziri wa Nchio ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) Hawa Ghasia,  baada ya serikali kukubali kulipa  mkopo  uliokopwa na halmashauri hiyo,  Benki ya biashara ya Afrika(CBA) kiasi cha sh 8.6 bilioni pamoja na riba sambamba na kurejesha gharama za mradi huo kiasi cha sh 788.2 milioni na faida ambayo halmashauri hiyo, ingepata kiasi cha sh5.6 bilioni.

Akizungumza mara baada ya madiwani hao, kwa kauli moja kukubali kulitoa eneo hilo, Waziri Ghasia alisema Serikali imekubali kulipa gharama hizo, ili kuhakikisha inapatikana ardhi hiyo kwa manufaa ya Taifa zima.

“ndugu zangu kabla ya leo kuja hapa, tulikuwa katika kikao cha kutafuta muafaka wa jambo hilo ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu kiongozi na watendaji toka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali, Wizara ya Ardhi Maendeleo ya Makazi na wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa”alisema Waziri Ghasia.

Waziri huyo, pia  alisema Rais Jakaya Kikwete alikuwa akifuatilia kupatikana kwa ardhi hiyo na ameiondoa hofu halmashauri hiyo, kupoteza fedha ambazo tayari wametumia na ambazo wangepata kama wangetekeleza mradi huo.

Hata hivyo, kabla ya madiwani hao, kukubali kutoa ardhi hiyo, walitaka uthibitsho wa maandishi wa Serikali kukubali kulipa deni la benki na gharama zote, hoja ambayo ilikubaliwa na waziri huyo, ambaye alisema tayari aliandika barua kwa halmashauri hiyo kueleza jinsi watakavyorejeshewa fedha zao.

“jamani mimi ni mtu mzima siwezi kuja hapa kusema ahadi ambazo hazipo,ninawahakikishia mtalipwa na mimi tayari niliandika barua kuelezea jambo hili naomba muiamini serikali yenu ahadi hii sio yangu ni ya serikali”alisema Waziri Ghasia.

Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha,  Halfani Hida alisema mradi wa awali kama ungetekelezwa tayari walikuwa wamepima jumla ya viwanja  348 ambavyo vingegawanywa kwa wananchi na kuipatia  halmashauri hiyo mapato ya sh 13.3 bilioni, pia viwanja vya biashara  biashara vingeingiza mapato ya sh 1.7 bilioni huku maeneo ya huduma yalitarajiwa kuingiza sh 332.6 milioni.

“baada ya mauzo ya viwanja  tungepata sh 15.5 bilioni na hivyo baada ya kutoa gharama mbali mbali  ikiwepo mkopo wa bemki ,halmashauri ingepata kiasi cha sh 4.9 bilioni”alisema Hida.

Eneo hilo la laki laki lina ukubwa wa ekari,  430 lilinunuliwa na halmashauri hiyo toka kwa Valahala Estate limited kwa sh 8.6 bilioni lakini wakati mradi ulipotaka kuanza ndipo mgogoro uliibuka baina ya halmashauri na watendaji wa serikali nje ya halmashauri na ndipo baadaye eneo hilo lilitwaliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya makazi  ambao ili kuchukuliwa na wizara ya mambo ya nje

TAARIFA IMEKUJIA KWA HISANI YA JAMII BLOG – PAMELLA MOLLEL

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO