Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HAPPY JOSEPH : MAMBO MATATU YANAYOWEZA KUHATARISHA AMANI KATIKA FAMILIA ZETU NA NCHI KWA UJUMLA

happy


KWA HESHIMA KUBWA NAPENDA KUWASHIRIKISHA MAMBO FULANI AMBAYO KIMSINGI YAWEZA KUHATARISHA AMANI KATIKA FAMILIA ZETU NA NCHI YETU KWA UJUMLA.
YAPO MAMBO MATATU ILA NITAANZA NA JAMBO MOJA MOJA ILI TUWEZE KUJADILI KWA UPANA WAKE… anaanza kueleza Happy Joseph (pichani). Endelea kusoma andishi lake..

KWANZA NITAANZA NA "UBINAFSI"
UbInafsi ni hali ya mtu, kujipendelea zaidi kuliko mwingine,
Hali ya kutaka kufaidi zaidi kuliko wengine- UMIMI. Mtu kusema, mimi kwanza, nitapata nini hapa, nakadhalika

Katika familia kama yupo mwanafamilia ambaye atajipendelea, lazima ataiangamiza familia yake. Iikiwa mama/baba ataweka maslahi yake binafsi mbele zaidi kuliko watoto na mume/mke wake, lazima ataleta maafa ktk nyumba yake, atapoteza amani ktk nyumba yake.

Mfano, baba aamue kutumia pato lake kunywa au kutumia na rafiki zake wakati mke na watoto hawana nguo, au mama aamue kutumia pato lake kununua mapambo yake wakati watoto na mumewe wanataabika, ugomvi hautakauka katika familia

UBINAFSI hauishii hapo, unaenda mbali zaidi, kutoka kwenye ngazi ya familia hadi nchi.
Mtu mbinafsi anapopata nafasi fulani huendeleza ubinafsi wao, na wakati huu hutumia mali ya walipa kodi kwa maslahi binafsi

Mfano mtu anaiba mali ya umma MAMILIONI YA FEDHA anaamua kwenda kuificha nje ya nchi, wakati kuna watanzania wanalala njaa. Mwingine anadiriki kusema kuwa ana VJISENTI wakati kuna watanzania wanakufa kwa kukosa huduma ya afya.

Huu ndio UBINAFSI. Wanaoficha fedha nje wanazisaidia nchi walizoweka fedha huko kujiendeleza kiuchumi wakati nchi ya Tanzania inateketea

Katika hali ya kawaida, unapojenga kisima kikubwa cha maji, bomba la kuingiza maji kisimani lazima liwe kubwa na la kutolea lazima liwe kubwa. Kama la kuingiza maji kisimani ni kubwa na la kutotea maji ni dogo, kisima lazima kipasuke.

Namaanisha, mtu mbinafsi hudhani kuwa amefaidika sana kwa mali alizochuma, lakini laana huikuta nyumba yake.

Mfano, tazama familia za watu wabinafsi, waliojilimbikizia mali, familia zao huishia kubaya.

DALILI ZA KUJUA NCHI INA WABINAFSI
Je, kuna wazee wangapi wanaokataa kustaafu ili maovu yao yasijulikane?
Je ni vijana wangapi wenye sifa za kupata ajira hawana ajira kwa kuwa wapo watu wamepeana ajira kinyemela?
Je, Viongozi wangapi wanatibiwa nje kwa kuwa Tanzania haina huduma nzuri za afya?
Je watoto wangapi wa vigogo wanasoma katika shule za kata?
Je ni mikataba mingapi imefanywa na viongozi wetu yenye kuumiza watanzania wote kwa maslahi yao binafsi?
Je watu wangapi hununua ardhi za majirani zao maskini kwa hila ili wapate eneo la kupak magari yao?
Je walimu wangapi wanafundisha kwa moyo?

IPO MIFANO NA DALILI NYINGI ZA UBINAFSI NCHINIUBINAFSI UMEZUA CHUKI ZA NDANI KWA NDANI KATIKA MIOYO YA WATANZANIA WALIO WENGI
Jiulize
Kijana aliyekosa ajira atampendaje yule aliyeipata kwa hila?
Je, nani atamfurahia aliyedhulumu ardhi yake? nakadhalika
NAWAACHIA NINYI WATANZANIA WENZANGU MSHAURI NINI KIFANYIKE

JAMBO LA PILI NI “” ANASA””
Anasa ni hali ya kutaka vitu vizuri, raha/furaha ipitayo kiasi, starehe….na kama jina la ANASA lilivyo, mpenda ANASA hunasa

Nitatoa mfano wa inzi katika asali
Inzi anapotua katika asali huanza kufyonza kwa muda, na kama tuwajuavyo inzi, hupenda kuinua miguu ya mbele au nyuma kushukuru Mungu (Dhana)
Akiwa kwenye asali baada ya kufyonza kwa muda hutamani kuinua miguu ya nyuma lakini kwa kuwa asali hunata, basi hushindwa kufanya hivyo na hujiambia…’nitashukuru baadaye’ kisha huendelea kufyonza

Baaya ya muda hutaka kuiinua ile ya mbele ambayo nayo inakuwa imenasa katika asali hivyo huahirisha na kujisemea….’nitashukuru baadaye’

Inzi huendelea kufyonza na baada ya muda huanza kusikia ubaridi tumboni…..kumbe tumbo limekuwa kubwa hadi kuigusa asali! Mwishowe tumbo hupasuka na inzi hufia palepale!!!!
Ukianza maisha ya ANASA si rahisi kujitoa, mpenda anasa yupo radhi kupoteza vyote lakini apatestarehe

NAMNA GANI ANASA YAWEZA KUWA TISHIO LA AMANI KATIKA FAMILIA NA NCHI
Katika familia, mwanafamilia yeote akiendekeza ANASA, lazima aangamize familia
Mfano, baba akiamua kuwa na nyumba ndogo/kimada, lazima apunguze huduma kwenye familia , na pia hawezi kuwa na upendo kama mwanzo…’huwezi kutumikia mabwana wawili’
Mke akigundua huweza kuleta fujo, kwa kimada, ndipo tunakutana na visa vya kujinyonga, kumwagiana maji moto, kutafuta vibaka wa kumkomesha mwenye tabia mbovu nakadhalika

Matendo haya huleta uvunjifu wa amani, na maelewano katika jamii
Hakuna mtanzania asiyejua kuwa nchi hii hutegemea kodi nyingi kutoka kwenye bidhaa za ANASA. Pia watanzania wengi tumezama katika ANASA inatutufanya tushindwe kukumbuka mambo ya msingi katika maisha

Kuna watu wana majumba ya kifahari, magari, na wanatumia hela zao kununua wanawake /wanaume-mashoga kwa ajili ya kustarehe, wengine huamua kuchezea fedha zao kamari. Kweli ni fedha waliyuichuma wao, pengine kwa jasho, pengine kwa udhalimu
Kwa kuwa watanzania timeendekeza ANASA, pombe zinazotengenezwa zinaua, UKIMWI nao unatuangamiza, lakini kwa kuwa tumesimama juu ya Asali hatuwezi kuona, kwa kuwa tumenasa.
Utamkuta mwanamama kasuka nywele za laki moja, wakati jirani yake mjane hana elfu ishirini ya ada za mwanae

Mbunge anatumia laki kadhaa kununua Malaya DODOMA wakati kuna yatina hana kaptula ya shule ya shilingi elfu kumi katika mtaa anaoishi, Mwingine anatumia laki kadhaa kununua pombe kwa usiku mmoja wakati jirani yake amelala kwa njaa!!! Haya ni maangamizi kwa taifa

Serikali inaweka bajeti kubwa ya kununua mazulia mapya, fanicha, viti vya kuzunguka, viyoyozi katika maofisi yao wakati hakuna DAWA HOSPITALINI, WALIMU HAWANA MSHAHARA…-ANASA

Je unategemea mwalimu afundishe kwa bidii wakati anasimama kutwa kwashulingi 6700 kwa siku wakati mbunge analalia kiti cha kuzunguka bungeni kwa shilingi laki mbili kwa siku??? Lazima mwalimu atafute namna ya kukomoa serikali…..maanganizi kwa taifa….

Robo tatu ya bajeti ya serikali yetu inaingia kwenye manunuzi ya vitu vya ANASA wakati watanzania hawana elimu bora wala maji, wala umeme!!! SERIKALI IMEJAA ANASA

DALILI KUWA NCHI IMEJIINGIZA KATIKA ANASA
• UNYWAJI POMBE UMEONGEZEKA
• BAJETI YA SERIKALI IMEYAPA KIPAUMBELE MAMBO YA ANASA ZAIDI KULIKO MAMBO YA MSINGI, mfano, rada, ndege ya rais n.k
• POMBE ZA AINA MBALIMBALI ZIMEONGEZEKA
• MATUMIZI YA MADAWAYA KULEVYA
• KUONGEZEKA KWA MAJUMBA YA STAREHE
• KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA UUZWAJI WA NGONO
• N.K
WATANZANIA WENZANGU, NCHI YETU IMENASA KWENYE ANASA
VIONGOZI WETU WAMETAWALIWA NA ANASA NA WAMENASA
ANASA HII IMEPANDIKIZA CHUKI BAINA YA VIONGOZI WAENDEKEZA ANASA NA WATANZANIA WALIPA KODI WENYE KUKOSA HUDUMA BORA ZA KIJAMII KWA KUWA KODI ZAO ZINATUMIKA KUWAPA RAHA VIONGOZI
Je, tufanye nini ili kuinasua nchi hii kwenye mikono ya wapenda ANASA?
Kesho tutaendelea na sehemu ya tatu na ya mwisho

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Anonymous said...

ukweli mtupu amani itapatikana wapi? wakati watu wana njaa.

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO