Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mauaji Ya Daud Mwangosi: Mkurugenzi wa Vilabu Vya Waandishi Wa Habari Aongelea Kinachofuata..

 

Watanzania wenzangu,nachukua fursa hii kuwajulisheni kuwa sisi viongozi wa UTPC,tunakichukulia kitendo hiki katika daraja ya aina yake na katu hatutanyamaza kama baadhi watu wanavyodhani.Hili ni shambulio la kwanza katika historia ya tasniaya habari Tanzania ambapo mwandishi wa habari anakufa mikononi mwa mwa maafisa wa umma,anauawa akiwa kazini.Sasa kwanza tumemtuma Rais wetu Kenneth Simbaya aende huko kulikotokea tukio hili na kufanya uchunguzi ambao utatupa picha kamili na ataileta taarifa hiyo kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC kitakachofanyika trh 5 sep.Kwenye kikao hicho tutatoa msimamo juu ya jambo hili.Kwa sasa nnawaomba Wastanzania wenzangu,waandishi wenzangu tutulie,lakini nawaambia Hamkani si shwari tena tena.

Wakatabahu,

Abubakar Karsan

Mkurugenzi Mtendaji

Union of Tanzania Press Club

Sourced from Mjengwa Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO