Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Vyama vya Siasa Vyawasilisha Maoni Yao Kuhusu Katiba Mpya Leo

Chadema wawasilisha maoni yao Katiba Mpya

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Januari 7, 2013.

Chenge akiwasilisha maoni ya CCM Tume ya KatibaMmoja wa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliofika katika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo. Viongozi hao pia walipata fursa ya kutembelea Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) na Kitengo cha Utafiti. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya chama hicho kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume jijini Dar es Salaam leo

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na uongozi wa NCCR-Mageuzi uliofika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid na kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Ndg. James Mbatia.

Kiongozi wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Ndg. Dominata Rwechungura akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA) Ndg. John Chipaka akimkabidhi Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ndg. Mwatumu Malale maoni ya chama chake kuhusu katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.

Chanzo: Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO