Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JK Ashuhudia uwekwaji wa Wakfu KKKT Singida

Rais Jakaya Akisalimiana na Askofu Malasusa

Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Januari 6, 2013, ameungana na mamia ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kushuhudia uwekwaji wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mteuli Dkt. Alex Seif Mkumbo kuwa Askofu mpya wa Dayosisi ya Kati ya Kanisa hilo.

Katika sherehe kubwa iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Imanuel mjini Singida, Rais Kikwete pia ameshuhudia kusimikwa kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mchungaji Syprian Yohanna Hilinti.

Rais Kikwete ambaye aliwasili mjini Singida j, Jumamosi, Januari 5, 2012 kwa ziara ya siku mbili za kikazi katika Mkoa wa Singida, amewasili kwenye Kanisa hilo kiasi cha saa nne unusu asubuhi na kupokelewa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Mkuu Dkt. Alex Gehaz Malasusa na mamia kwa mamia ya waumini waliohudhuria ibada na sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu.

Askofu Mkumbo na Mchungaji Hilinti wanachukua nafasi za Askofu Eliuphoo Yohana Sima na Mchungaji Yohana Ramadhani Mujungu na walichaguliwa kushika nafasi hizo katika Mkutano wa Uchaguzi (SINODI ya 12) wa KKKT Dayosisi ya Kati uliofanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu Imanuel, Singida, Juni 27 hadi 29 mwaka jana, 2012.

Katika sherehe zilizofanyika jana na kuhudhuriwa pia na viongozi wa Serikali na wageni kutoka nje ya nchi, Askofu Mkumbo amepitishwa katika hatua mbili ili kukamilisha nafasi yake kama Askofu wa Jimbo la Kati na Mkuu wa KKKT katika Dayosisi hiyo.

Katika hatua ya kwanza, Askofu Mteule Mkumbo aliwekwa wakfu wa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Kati ya KKKT katika shughuli iliyosimamiwa na Askofu Dkt. Martin Fuataeli Shao, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini akisaidiwa na Askofu Charles Robson Mjema, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Pare na Askofu Dkt. Hans-Jurgen Abromeit, Mkuu, Pomeranian Evangelical Church (Lutheran Church in Northern Germany).

Kwa nafasi yake hiyo, Askofu Mkumbo anakuwa mwangalizi wa shughuli zote za Dayosisi pamoja na maisha ya kiroho katika Dayosisi. Aidha, anakuwa msimamizi wa huduma ya kichungaji na maisha ya familia ya kiuchungaji.

Katika hatua ya pili, Askofu Mkumbo amesimikwa kuwa Mkuu wa KKKT katika Dayosisi ya Kati shughuli ambayo imefanywa na Mkuu wa Kanisa KKKT Askofu Mkuu Dkt. Malasusa. Nafasi hii inampa Askofu madaraka kamili ya utawala na uendeshaji wa Dayosisi na kuwa wakili mwema wa mali zote za Dayosisi

Baada ya shuguli za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mkumbo, naye katika nafasi yake mpya amemsimika Msaidizi wa Askofu, Mchungaji Syprian Yohana Hilinti.

Dkt Kikwete Ahudhuria Kusimikwa Wakfu Askofu Dkt Mkumbo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi hiyo huku Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013

CHANZO: THE HABARI.COM

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO