Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbinu za Wizi Wa Kura Hizi Hapa

ballot-box

  • Kuhonga mawakala wa vyama vingine kwa gharama yeyote ili kuruhusu matokeo kubadilishwa. Hili linadhibitika ikiwa mawakala watasimamia maadili ya uwakilishi wa vyama vyao kwa uaminifu bila kutanguliza njaa.
  • Kuweka vituo hewa vya kupigia kura, hasa katika maeneo ambayo si rahisi mwananchi wa kawaida anaweza kuhoji i.e kwenye kambi za jeshi n.k. Pia kunaweza kuwekwa vituo hewa ambavyo vinakuwa na majina hewa mengi huku wapiga kura wengi wakishindwa
    kupiga kura.
  • Kuukimbia na masanduku ya kura..
  • Ushiriki wa vyombo vya kiserikali vyenye dhamana ya kusimamia haki, lakini badala yake vinaamua kuwa upande wa chama kinachotaka kushinda kwa wizi. Mfano Tume ya Uchaguzi n.k
  • Kununua shahada za kupigia kura ili waliouza shahada zao wasiweze kuwa na ruhusa ya kupiga kura.
  • Kutumia Polisi kutisha wapiga kura kwenye zoezi la kupiga kura na hata wakati wa kuhesabu kura.
  • Kusambaza Form chache sana kwenye vituo, zile fomu zinazoruhusu asie na kitambulisho ama kimeharibika details fulani aruhusiwe kupiga kura. Ni rahisi kuambiwa hizo form hazipo au hazijaletwa kituoni.
  • Kuondoa baadhi ya majina ya wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.
  • Kuharibu majina ya wapiga kura yaonekane yamekosewa ama hayafanani na picha ya mhusika
  • Kubandika majina siku chache sana kabla ya siku ya uchaguzi, muda ambao hauwaruhusu ambao majina yao hayapo au yamekosewa kuweza kufanya marekebisho
  • Kuchanganya majina ya wapiga kura na vituo. Mfano aliejiandikisha kituo A, jina lake unalikuta kituo B na pengine ikawa ni mbali sana na anapoishi
  • Kuingiza maboksi yaliyojaa kura zilizopigwa tayari za chama kinachotaka kuiba, aidha wakati wa kusafirisha ama wakati zimefungiwa ndani. hii ya wakati wa usafirishaji inawawia ugumu kwasababu mfumo wa kuhesabia kura kila kituo unaleta shida.
  • Wakati mwingine kura zikihesabiwa katika jengo ambalo lina ceiling kwa ndani wanaweza kuwaambia mawakala kwenda kupata chakula na milango inafungwa vizuri lakini kumbe kwa juu ya dari anakuwepo mtu alieandaliwa na mabox yake yenye kura ambazo zimepigwa, nyingi zikiegemea upande wa chama kinachotaka kuiba, mawakala wkiwa nje wanakula yule mtu darini anashuka na kuweka zakwake zilizoandaliwa.
  • Usalama wa nchi wakati mwingine unaweza kuhusika moja kwa moja katika wizi kwa kutumia nafasi yao ya kusimamia usalama, kwa kuvujisha siri za mwenendo wa uchaguzi! 
  • Mbinu nyingine ambayo huwa wanaitumia ni kujífanya wema sana kwa wakala hasa yule wa chama ambacho kina nguvu, kwa kumpatia chakula ambacho akila tumbo linavurugika na anaanza kwenda chooni mara kwa mara na wao kutumia nafasi hiyo kuweka kura zisizo rasmi.
  • Kunayo taarifa za kuwako mbinu mpya ya kiteknolojia kwa zile fomu za majumuisho. Inaelezwa kuwa hii ndio mbinu kuu iliyo na nguvu kwasababu mara nyingi mawakala wakishasaini fomu moja na kubakia na kopi moja wanadhani wamemaliza. Ila wakati zinapelekwa kwenye majumuisho zinakuwa sio zile walizosaini mawakala. Kunakuwa na fomu nyingine kama ile ile lakini inajazwa pembeni!!
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO