Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HOTELI YA NAURA SPRING YA ARUSHA IKO HATARINI KUBOMOLEWA

Chanzo: Tanzania Daima, Machi 14, 2012

na Ramadhani Siwayombe, Arusha

 

SAM_1750 NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye, ametoa agizo kwa Mamlaka ya Uhifadhi wa Mazingira nchini (NEMC), kufika mkoani Arusha na kuchunguza ujenzi wa Hoteli ya Naura Spring ambayo inadaiwa kujengwa kwenye chanzo cha maji.

Endapo hoteli hiyo maarufu nchini itabainika kujengwa kwenye chanzo cha maji, inaweza kubomolewa ili kuruhusu upatikanaji wa maji katika Jiji la Arusha ambao kwa sasa umepungua kutokana na ujenzi holela na uharibifu wa mazingira.

Hoteli hiyo maarufu kwa shughuli mbalimbali za mikutano ya kitaifa na kimataifa mkoani hapa inadaiwa kujengwa katika chanzo cha chemchemi ya maji na kusababisha ukosefu mkubwa wa maji kwa wakazi wa mkoa huo.

Waziri Medeye alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa maji Mkoa wa Arusha, unaofanyika katika hoteli hiyo maarufu ya Naura Spring.

Alisema kuwa hivi sasa Arusha inakabiliwa na tatizo kubwa la maji kutokana na ujenzi unaofanywa bila kuwa na usimamizi thabiti wa watendaji na hivyo kuchangia uharibifu wa mazingira na kuharibu vyanzo vya maji.

Alifafanua kuwa hali hiyo imeifanya Arusha kupoteza hali yake ya zamani ambapo mito mingi ilikuwa ikitiririsha maji kipindi chote cha mwaka mzima na wakati mwingine kusababisha mafuriko.

Alisema kutokana na uharibifu huo ameagiza pia halmashauri tatu za Meru, Arusha na Jiji la Arusha kushirikiana na kuhakikisha inapima ardhi yote ya makazi ili kudhibiti ujenzi holela unaopelekea uharibifu wa vyanzo vya maji.

”Nasisitiza kuwa ardhi yote ya makazi si kwa lengo la kuwanyangánya wamiliki wake bali tuwe na uwezo wa kudhibiti ujenzi lakini pia kuwawezesha wananchi pindi wanapotaka kujenga iwe ni lazima kuomba kibali na wahusika kuthibitisha kile kinachotaka kufanyika,’’ alisema Naibu Waziri Medeye.

Awali kabla ya kufungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA), Felix Mrema alitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji safi katika Jiji la Arusha kuwa imeshuka kutoka asilimia 98.5 iliyokuwepo zamani na kufikia asilimia 44 hivi sasa.

Alisema hali hiyo imetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maji kunakotokana na kupungua kwa vyanzo vya maji kulikosababishwa na uharibifuwa mazingira.

Alisema kufuatia hali hiyo ndio maana waliamua kuitisha mkutano huo wa wadau ili kufikia maamuzi ya nini kifanyike kunusuru hali hiyo na kuwawezesha wananchi wa Arusha kupata maji safi na salama.

Nyongeza na arusha255
Kwa uhalisia wa mto unaotiririka nyuma ya hoteli hii, endapo wazo la kubomoa ili kulinda hifadhi ya mto litafikiriwa kufaniwa kazi na ikawa hivyo kweli, ni wazi kuwa zoezi hilo linapaswa kuathiri na majengo mengine yalijengwa kando ya mto huo kama vile Jengo la Benki Kuu tawi la Aruaha na ofisi za TRA Arusha.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO