Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA WAITEKA KIRUMBA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI, ZITTO AWASHA MOTO

Baada ya kushiriki kwa mafanikio makubwa katika uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki juzi eneo la Usa River, Arumeru-Arusha, jana MH Zuberi Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, alikuwa na kibarua kingine katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Udiwani Kata ya Kirumba- Jijini Mwanza.

Kata ya Kirumba ilikuwa wazi baada ya diwani wake wa awali, Novat Manoko (CHADEMA) kufariki dunia Agosti 30, mwaka jana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya shinikizo la damu.

Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili Mosi mwaka huu. Kwa ujumla zipo chaguzi ndogo 7 za Udiwani nchini na CHADEMA wanatarajiwa kushiriki chaguzi zote, taarifa ambayo imethibitishwa na mwenyekiti wa chama hicho hivi karibuni.

Zitto - Kirumba2

Zitto Kabwe akimwaga sera Kirumba, Jijini  Mwanza

Zitto - Kirumba1

Sehemu ya Umati uliojitokeza Kata ya Kirumba Jijini Mwanza

Zitto - Arumeru3

Hii ilikuwa juzi Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, Usa River Arusha mara baada ya mkutano kumalizika

Umati uliojitokeza kusikiliza hotuba..


Picha zote na Zitto Kabwe!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO