Pichani, Nadir haroub 'Canavaro" akitoka nje ya uwanja baada ya kulimwa kadi nyekundu
Ilibidi mwamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timuza Yanga ya Jangwani na Azam FC kutoka Chamazi uliofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam jana, Israel Mujuni pamoja na wasaidizi wake watoke nje ya uwanja kwa kusindikizwa na askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU mara baada ya kupuliza kipenga cha mwisho kumaliza mchezo huo ambapo Yanga ilikandamizwa magoli 3-1 na wauza ‘icecream’ hao wa Chamazi.
Mwanzo ulikuwa ni mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na kuingilia vurugu hizo.
Kwa picha na habari fuata hii link Burudani Mwanzo Mwisho Blog
0 maoni:
Post a Comment