Hatma ya Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini (CCM), Virajilal Jitu Son imefahamika leo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wake iliyofunguliwa na aliyegombea ubunge wa Jimbo hilo, Laurence Sharubu Tara (NCCR Mageuzi)
Mahakama imemruhusu Jitu Son kuendelea na Ubunge wake na kutupilia mbali maombi ya Tara, ambaye ni Diwani wa Kata ya Bashnet ya kuitaka Mahakama hiyo imtangaze kuwa Mbunge halali akidai kuwa alimshinda Jitu Son kwa tofauti ya kura 58.
Kesi hiyo namba 12/2010 ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Fatuma Massengi na ilifunguliwa Novemba 2010 na kuanza kusikilizwa February 16 mwaka huu huku wadaiwa wakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo na Mh Jitu Son.
0 maoni:
Post a Comment