Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAOFISA WA NEC WAJICHANGANYA SAKATA LA KUWAKO VITUO BANDIA 55 ARUMERU MASHARIKI

Chanzo: Mwananchi Habari

Tuhuma kwamba kuna vituo 55 vya bandia vilivyoandaliwa kwa lengo la kutumika kuiba kura kwenye uchaguzi huo, zinaonekana kugonganisha vichwa vya maofisa wa uchaguzi.


Tuhuma hizo ni zile zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa juzi kwamba kuna vituo 55 bandia 55 vya kupigia kura katika uchaguzi huo mdogo madai ambayo yalikanushwa na Msimamzi wa Uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi.

Juzi Kagenzi alipozungumza na waandishi wa habari alisema vituo halali ambavyo anavitambua ni 327 tu na hakukuwa na kituo ambacho kimeongezwa na kwamba hata kama ikitokea hivyo, itakuwa ni baada ya majadiliano na vyama vyote shiriki.
“Vituo vilivyopo ni 327 pekee, na kama ikitokea kituo kinakuwa na watu zaidi ya 500 ndipo kunaweza kuongezeka, lakini historia inajionesha kila uchaguzi mdogo unapofanyika idadi ya wapigakura inapungua,”alisema Kagenzi.


Lakini jana Kagenzi alikiri kuwapo kwa kasoro kwenye orodha ya vituo hivyo na kwamba alikuwa anawasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuwezesha kufanyika kwa marekebisho.


Maeleo ya Kagenzi yanatokana na ushahidi ambao gazeti hili liliupata kwa kuona orodha ya vituo hivyo, ambayo ilikuwa ikionyesha takwimu mbili tofauti za idadi ya vituo vya kupigia kura.

Katika orodha hiyo, safu ya idadi ya vituo vya kupigia kura katika kata 17 za jimbo hilo ilikuwa ikionyesha vituo 327, wakati safu ya mwisho ya orodha hiyo hiyo ilikuwa ikionyesha kuwapo kwa jumla ya vituo 382, likiwa ni ongezeko la vituo 55.
Waraka wa orodha hiyo unaonyesha kuwa katika Kata ya Akheri kutakuwa na vituo 20 idadi ambayo inayofautiana na iliyotolewa na tume ambavyo ni vituo  18.

Kata nyingine ambazo vituo hivyo vinaonekana kuongezwa ni Kikatiti vituo 22 badala ya 18, Kata ya Kikwe vituo 12 badala ya halali 11, Kata ya Kingori vituo 29 badala ya halali 26 na Kata ya Leguruki vituo 23 badala ya halali 20.

Kata nyingine ni Makiba vituo 21 badla ya halali 18, Majiya chai 24 badala ya 29 halali, Maroroni vituo 21 badala ya 17 halali, Mbuguni vituo 25 badala ya halali 21,Nkoarsambu vituo 10 badala ya 8 vinavyohitajika na Kata ya Ngarenanyuki ambako vimeongezwa vituo sita kutoka halali 20 hadi 26.

Orodha hiyo ambayo Kagenzi alithibitisha kwamba ilikuwa na makosa pia ina kasoro katika Kata za Nkoaranga ambako vituo vimeongezwa kutoka halali 17 hadi 22, Pori kutoka vituo halali 16 hadi 20, Nkwandua kutoka vituo 22 hadi kufikia 25 na Kata ya Seela - Sing’isi vituo hivyo viliongezwa kutoka halali 12 hadi 15.


Kata nyingine ni Songoro  nyumbani kwa Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari vipo vituo 15 na hakuna kilichoongezeka huku Kata ya Usa River ilikuwa na vituo 36, lakini vimeongezeka vitano na kufikia 41.


Kagenzi alisema alipowasiliana na idara ya teknolojia ya habari ya NEC kuhusu kasoro hizo walimwambia kwamba orodha ya awali haikuwa toleo la mwisho na kwamba wangefanya marekebisho ya kuondoa kasoro hizo.
“Wameniambia kwamba hiyo orodha ilikuwa ni working draft tu (rasimu ya kufanyiwa kazi), kwahiyo nimeomba hiyo orodha kamili ya mwisho, wakishanitumia nitaisambaza kwa vyama husika,”alisema Kagenzi jana.


Baadaye msimamizi huyo wa uchaguzi alisema wataalamu kutoka NEC walitarajiwa kuwasili Arumeru jana mchana kwa ajili ya kurekebisha kasoro hizo pamoja na kufanya maandalizi mengine kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.

Hata hivyo, kauli ya Kagenzi ilikuwa ikipishana na ile iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba ambaye awali alisema hakukuwa na vituo vya nyongeza kama ilivyodaiwa na Dk Slaa.
Baada ya kuelezwa kuhusu orodha hiyo ya tume, Mallaba alisema: “Basi kama iko hivyo nitawasiliana na wahusika ili tuone hatua waliyofikia katika kurekebisha kasoro hizo”.


Dk Slaa alisema hali kama hii waliibaini katika Jimbo la Igunga mara baada ya matokeo kutangazwa na baada ya kufuatilia walikuta vituo hewa ambapo vilikuwa na kura kati ya 160 na 280.

Nyongeza na ARUSHA YETU BLOG

Wakati Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Lubuva anakanusha kuwako ongezeko la vituo vya kupigia kura huko Arumeru, Msimamizi wa Uchaguzi Arumeru Mashariki Bw Kagenzi anakiri kuwa ni kweli kuna vituo vimeongezwa. Hizi ni taarifa za watendaji wawili muhimu kwa demokrasia ya kweli, na kauli zote zimetolewa siku moja, jana! Hii inaashiria tatizo mahali fulani.

Tume ya Uchaguzi ndiyo imebeba dhamana ya amani na haki kwa watanzania katika kupata viongozi wao. Ni tume ya vyama vingi na sio ya chama kimoja, hivyo ni shatri ionekane ikitenda kwa sifa hiyo. Katika maeneo mengine kunakotokea vurugu mara baada au hata kabla ya uchaguzi huwa ni matokeo ya haki kutotendeka kwa mamlaka zinazosimamia haki kushindwa kutenda haki!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO