Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rais Kikwete Amuapisha Mkuu Mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba Ikulu jijini Dar

8E9U5294Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi Machi 19.12. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria

8E9U5299  Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi mkuu mpya wa JKT meja Jenerali Samwel Ndomba wakati wa hafla ya kumuapisha iliyofanyika jana asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam

8E9U5326Amiri Jeshi mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange(kushoto) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana.

8E9U5309  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,(kushoto)Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha mkuu huyo mpya wa JKT Ikulu jijini Dar es Salaam jana

8E9U5331 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mzee Albert Ndomba(85),baba mzazi wa Mkuu Mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba(wapili kushoto) baada ya halfa ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana .Kulia ni mke wa Meja Jenerali Ndomba na waliosimama nyuma ni wanafamilia

Picha&Maelezo: Daily Mitkas Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO