Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA Yaomba Kuungwa Mkono Kiuchumi Kuleta Mabadiliko Ya Kweli

DSCN0113 Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimeanzisha utaratibu wa kuwaungunisha wananchi ili kushiriki moja kwa moja katika harakati kuleta mabadiliko ya kweli nchini.

Akizungumza jana katika ufunguzi wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari kwa uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki unaotarajiwa kufanyika Aprili 1, Mwenyekiti wa chama hicho ambae pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe alisema CHADEMA inapenda kumshirikisha kila mwananchi, mpenda maendeleo na yeyote mwenye mapenzi mema na Taifa la Tanzania kukichangia chama hicho kiasi chochote atakachoweza kuwa nacho ili kugharamia juhudi za kuleta mabadiliko ya kweli.

Mbowe alisema CHADEMA hakiwezi kufanya siasa ya kutanguliza fedha kama wengine wanavyofanya, siasa ambayo alidai ni siasa chafu ambayo haiwezi kulisaidia taifa kwasababu wakati mwingine fedha hizo hutoka kwenye vyanzo vichafu ukiwemo ufisadi ambao ni dhuluma kwa wananchi.

Akizungumzia siasa inayotarajiwa Arumeru, alisema inahusisha pande mbili zinazokinzana, upande mmoja ukitumia fedha na mbinu chafu, dhuluma na matumizi ya nguvu za dola ili kuweza kushinda uchaguzi, na upande mwingine ukimtegemea Mungu tu.

Aidha, Mbowe aliueleza umma wa watanzania na ulimwengu mzima kwa ujumla, uliokuwa ukifuatilia hotuba yake kupitia Star Tv na Redio Sunrise ya Arusha, kuwa ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa ni utumwa hasa kwa vyama vya upinzani. Akadai kuwa hata kama serikali ikifuta ruzuku hizo, bado CHADEMA itatumia ruzuku yawananchi na hivyo kuwaomba watanzania kuichangia CHADEMA kwa ajili ya ukombozi wa taifa.

Akitaja namba za simu kwa makampuni tofauti yenye kuwezesha huduma ya fedha nchini, ambazo wananchi watazitumia kutuma michango yao, alisema angependa kuona watanzania wakianza kushiriki harakati za ukomozi nchini kwa kuanza na uchaguzi wa Arumeru Mashariki.

Namba hizo ambazo zote zimesajiliwa kwa jina “Chadema Arusha” alizitaja kuwa ni MPESA 0757 755 333, 0763 744 334, 0763 766 333, na 0758 003 509. Kwa upande wa AIRTEL MONEY ni 0684 424 229, 0684 424 144, na 0684 425 222.

Nyingine ni TIGO PESA, 0655 788 333, 0718 611 168, na 0718 611 126.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO