Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MSHINDI WA SAFARI LARGER NYAMA CHOMA (ARUSHA) APATIKANA

Bar ya ROYAL STOPOVER iliyopo maeneo ya Kwamrefu Jijini Arusha imeibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia kitita cha sh 1,000,000/= katika mashindano ya uchomaji nyama kwa kanda ya Arusha yaliyofanyika jana viwanja vya Kaloleni, kwa kuratibiwa na kudhaminiwa na Tanzania Breweries Ltd kupitia bia ya Safari.

Jumla ya sh 3,000,000 zilitolewa kwa washindi wa kwanza hadi watano, pamoja na vyeti maalumu kutambua ushiriki wa wachomaji nyama tofauti tofauti waliojitokeza kushiriki.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa Arusha Night Park ya Mianzini (sh 800,000/=), nafasi ya tatu walikuwa 2i Pub ya Kijenge Chini (sh 600,000/=), nafasi ya nne Rombo Delux (sh 400,000/=), na washindi wa tano walikuwa Mjengoni Club ambao walijinyakulia sh 200,000/=.

Akitangaza washindi hao, Jaji wa mashindano alisema vigezo vilivyotumika kupata washindi viliangalia usafi binafsi na wa vyombo vilivyotumika, jiko na namna ya uchomaji, usalama wa wachomaji na walaji, na namna nzuri ya kumhudumia mteja.

DSCN0281Washindi wa kwanza – Royal Stopover

DSCN0308Mshindi wa kwanza (Royal Stopover) akipokea zawadi ya sh 1,000,000/= kutoka kwa meneja wa bia ya Safari Arusha

DSCN0283Washindi wa pili – Arusha Night Park ya Mianzini

DSCN0280Banada la washindi wa tatu –2i Pub

DSCN0276Washindi wa nne –Rombo Delux

DSCN0279Banda la Mjengoni Club, washindi wa tano

DSCN0293Washindi wa pili, 2i Pub wakiserebuka uwanjani  mara baada ya kutangazwa

DSCN0296Kiongozi wa 2i Pub akifurahia zawadi ya laki nane

Picha zote na Tumainiel Seria  

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO