Taarifa za jioni hii kutoka Arumeru Mashariki zinasema vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, hususani washindani wakuu, CHADEMA na CCM vimewekeana mapingamizi kwa wagombea wao.
CHADEMA kwa upande wao kimemuwekea mapingamizi takriban manne mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Sioi Sumari kwa madai kwamba si raia wa Tanzania, na tuhuma nyingine za rushwa.
Vyanzo vya taarifa vinadai CHADEMA imenasa barua ya siri yenye Kumb No.AR/C/32/VOL1/85,ya Feb 29/2/2012,kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa uhamiaji mkoa wa Arusha,kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha,ikifafanua uraia wa Sioyi,na katika ufafanuzi huo Ofisi ya uhamiaji inakiri kuwa kwa yeyote aliyezaliwa nje ya nchi,ukomo wa uraia wake ni pale anapofikisha miaka 18,na baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alipozaliwa.
Nao CCM wamemuwekea pingamizi moja mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari kuhusiana na kazi yake kwamba, Nassari ana taaisisi inayofanya kazi wakati haijasajiliwa!
Nae mgombea ubunge kupitia UPDP amemuwekea pingamizi mgombea wa CHADEMA, joshua Nassari kwa madai kuwa fomu yake haijajazwa inavyotakiwa. Pingamizi linaeleza kuwa katika fomu ya Nassari, jina la chama chake limeandikwa kwa kifupi badala ya kuandikwa kwa marefu yake.
Wagombea wote waliowekewa pingamizi wanatakiwa kuwasilisha utetezi wao kabla ya saa 10 jioni, kesho.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment