Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UCHAGUZI WA WAJUMBE 9 WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA APRIL 17 DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

____________

Katibu wa Bunge anatoa Taarifa kwa Umma kwamba, Uchaguzi wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba utakaofanyika Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012.

Uchaguzi huo wa Wabunge wa  Bunge la Afrika Mashariki unafanyika kwa kuzingatia kuwa maisha ya Bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2006, yatafikia ukomo wake  04 Juni, 2012.

Pamoja na Taarifa hii, Katibu wa Bunge ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi huo, atatoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa masharti yanayohusika, kuhusu siku ya uteuzi, ambayo ni tarehe 10 Aprili, 2012, saa kumi (10.00) Jioni, na pia kuhusu siku ya uchaguzi ambayo ni tarehe 17 Aprili, 2012 saa tano (5.00) Asubuhi, mara au mapema baada ya Kipindi cha Maswali. 

Aidha, katika Tangazo hilo, Katibu wa Bunge pia atatoa masharti yanayopaswa kuzingatiwa na Wagombea wa Vyama vyote vya Siasa vyenye uwakilishi Bungeni kuhusiana na Uchaguzi huo, kwa ajili ya  kuviwezesha kuanza mchakato wa kuwapata Wagombea kupitia Vyama hivyo, ambao majina yao yatawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura.

Kwa Taarifa hii, watu ambao wanazo sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wanaweza kuanza mchakato wa kuteuliwa kuwa wagombea wa uchaguzi huo, kupitia Vyama vyao vya Siasa.

Taarifa hii imetolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO