Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

VICENT NYERERE AMLIPUA TENDWA

mkapa na vicent Vicent Nyerere amemshukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kwa kumzuia kumzungumzia Hayati Mwalimu Nyerere.

Amemshauri kuwa kama anahitji kuwa mmoja wa familia yao, anaruhusiwa kuandika barua kuomba kujiunga na ukoo wao kama alivyofanya Mkapa.

Alisema anamshangaa Tendwa kumpiga marufuku kuongelea mambo ya baba yake na kulidanganya Taifa kuwa watahatarisha amani nakujenga chuki kwa Taifa kwa kumzungumzia Nyerere.

“Mimi huyu ni baba yangu na kila siku lazima nimtaje na sisi wakatoliki tuna sala maalum ya kumwombea Nyerere na leo (jana) pia nimesali mara baada ya kuamka, sasa yeye ni nani anayenizuia kutaja jina lababa yangu, kama anataka ajiunge na ukoo wetu aombe kwa barua, kama alivyofanya mwenzake Mkapa, aliandika barua akaingizwa katika ukoo,”alisema Nyerere.

Akimnadi Nassari katika mkutano wa hadhara wakampeni, Vincent Nyerere, ambaye ni Meneja wa kampeni za mgombea ubunge waChadema Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, jana alisema kuwa Mkapa amemfuata Joseph Butiku kuomba amuombea msamaha kwake (Vincent). Alisema kuwa Mkapa alimweleza Butiku kuwa alikuwa anamtania ingawa mbunge huyo aliichukulia kauli ya Rais huyo mstaafu kama ya kweli.

“Huyu Butiku jana (juzi) alinipigia simu akiniomba tuachane na haya mambo ya malumbano kwa sababu Mkapa alikuwa ananitania na hakujua kama itakuwa hivyo, na mimi nimeendelea kulisema hadharani, sasa anaomba basi yaishe,”alisema Nyerere katika mkutano uliofanyika katikakijiji cha Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni.

Alisema kuwa amekataa kuombwa radhi kupitia njia yasimu au kukutana wawili na kuongeza kuwa anachotaka ni Mkapa kwenda Arumeru kuomba radhi katika mkutano wa hadhara ambao aliuhutubia na kumchafua kuwa hanaundugu na Hayati Mwalimu Nyerere.

Aidha, alisema Mkapa anapaswa kuwenda kumuomba radhi kwenye ukoo wao. “Mimi ni wa ukoo wa Nyerere atake asitake, Nyerere ni baba yangu na sitaacha kumtaja kamwe,” alisema Vincent.

Alisema kuwa Mkapa alikuwa anamheshimu sana kama Rais mstaafu na alifahamu anahitaji kupumzika, ila kwa kumgusa kwa hilo nakumchafua hadharani kuwa anajifanya mtoto wa Nyerere, wakati hamfahamu, kwa hilo aende katika ukoo kumsafisha.

Chanzo: maelezo –Nipashe, picha na Mjengwa Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO