Kjana aliejitambulisha kama afisa mpelelezi wa Polisi (mwenye shati jeupe katikati) akiwa amezongwa na wananchi Mtaa wa Disemba, mako mapya Arusha, Jumamosi
Kijana mmoja aliejitambulisha kama afisa wa Polisi toka makao makuu ya Polisi Arusha, aliejitambulisha kwa jina moja la Bosco, alijikuta katika wakati mgumu pale alipoanzisha ukaguzi wa kipelelezi kwa gari aina ya RAV4 lenye namba T530 BCT linalomilikiwa na mwanachama wa chama CHADEMA kwa lengo la kutaka kuthibitisha uhalali wa umiliki wake.
Tukio hili lilitokea siku ya Jumamosi Machi 17 na kuvuta watu wengi kushuhudia, katika eneo maarufu mjini Arusha kama Mtaa wa Disemba, Makao Mapya mahali ambapo gari hilo lilikuwa limeegeshwa.
Gari iliyoleta kizaazaa kwa mbele pichani, nyuma wananchi wakimsikiliza “afisa mpelelzi”
Mashuhuda wa mkasa mzima wanasimulia kuwa kijana huyo alifika eneo hilo na kujitambulisha kama afisa wa Polisi na anahitaji kuchunguza kama gari hilo kama linamilikiwa kihalali kwasababu alidai kuna mtu Morogoro analalamika ameibiwa gari kama hiyo.
Baada ya kupewa nyaraka zote za umiliki, na kukuta gari linamilikiwa kihalali, aligeuza kibao na kudai yeye ni afisa wa TRA na hivyo anahitaji kuona kama road licence imelipiwa.
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya watu walimzonga na kumuweka kati ili aeleze lengo hasa nini kwa maana alionekana kukosa msimamo wa kile alichokuwa anakitaka. Ni bahati nzuri kwake alitokea msamaria mwema akamwombea asipewe kipigo.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuona hali inamuelemea kiasi cha kuhatarisha usalamawake, alipiga simu kwa wenzake, na mara ikaja Defender yenye askari, wakaja na kumtetea kisha wakamchukua na kuondoka nae na kuiacha gari ile pale pale!
Hapa akiandika namba ya gari, wakati huo amedai ni afisa wa TRA na sio afisa mpelelzi wa Polisi tena.
Aidha, baadhi ya mashuhuda walihusisha tukio hilo na kampeni za uchaguzi zinazoendelea huko Arumeru Mashariki ambako kuna ushindani mkubwa baina ya washindani wakuu Chama Cha Mapinduzi CCM na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Kulihusisha tukio hili na kampeni za Arumeru kunatokana na ukweli kwamba gari hiyo huwa inatumika katika shamrashamra za mikutano ya CHADEMA na jinsi lilivyo, muda wote huzurula mjini na bendera ya CHADEMA huku likiwa na maandishi makubwa kila upande ya kukinadi chama hicho.
0 maoni:
Post a Comment