Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA leo kimefanya mikutano mitatu kama ilivyo ratiba yake ya kila siku kwa kamapeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki. Hii ni mbali na kampeni nyingine za nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa zinazoendelea Jimboni humo.
Siku ya leo walifanya mkutano wa kwanza Kikatiti na wa pili eneo la Nkoaranga Wilayani Arumeru, na mkutano wa mwisho ulifanyika eneo la stand mpya ya mabasi/vifodi eneo la Tengeru.
Mgombea wa chama hicho aliweza kuhutubia mkutano wa kwanza na wa pili lakini hakuweza kupatikana kwa mkutano wa tatu Tengeru kutokana na mabadiliko ya ghafla katika ratiba yake ya kampeni.
Pamoja na kutokuwepo kwa Nassari, bado mkutano wa Tengeru uliweza kufanyika kwa ufasisi mkubwa chini ya usimamizi na uhamasishaji wa Waitara Mwita Mwikabwe, Mch Msigwa na Mbunge wa Viti Maalumu Moshi, Mh Grace Kiwhelu, ambao ndio pekee waliohutubia mamaia ya watu waliojitokeza, sambamba na diwani mmoja wa viti maalumu kutoka Arusha Mjini.
Hali ya usalama ilikuwa ni tulivu sana na ya kutia matumaini, hakukuwa na kashkashi yoyote ile na mwisho mkutano ukamalizwa ndani ya muda uliokubaliwa. Picha chache zifuatazo zinaweza kuwa na maelezo zaidi…
Sehemu ya umati uliojitokeza uwanjani hapo leo..
Mchungaji Peter Msigwa, ambae pia ni Mbunge wa Iringa Mjini akihutubia
Wananchi wakishiriki ishara ya “Peoples Power”
Miselebuko nayo haikukosekana baada ya mkutano kuisha
Huyu dogo alikuwa kivutio sana…. Alipandishwa jukwani na kusalimia
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Monduli, Aman Ole Silanda (mwenye kofia) aka “mwarobaini wa Lowassa” alikuwepo uwanjani.
Ndie aliyekuwa mpinzani Mkuu wa Lowassa katika Uchaguzi wa 2010
Kamanda Mwikabwe Mwita Waitara akishuka jukwaani
Wamama hawa pamoja na kuwa busy na biashara hawakusita kushangilia msafara wa viongozi wa CHADEMA uliokuwa ukipita mbele yao baada ya mkutano kuisha
Jukwaa kuu halikuwa na wale wabunge machachari waliozoeleka…
Zoezi la uchangishaji ‘sadaka’ lilipita mpaka nje ya mkusanyiko, hadi kwenye mapumzikio ya abiria stand
1 maoni:
Ushindi upo upande wetu, Pipoz.....
Post a Comment