Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NSSF YAANDAA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA KWA JAMII BURE, ARUSHA MACHI 22

Shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii, NSSF kwa kushirikiana na Hospitali binafsi nchini wameandaa zoezi la upimaji afya kwa jamii linalotarajiwa kufanyika maeneo mbalimabli ya nchi, ambapo mjini Arusha zoezi litafanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kuanzia tarehe 22 hadi 23 Machi, 2012.

Baadhi ya matatizo ya kiafya yatakayoangaliwa siku hiyo ni pamoja na Kisukari, Shinikizo la damu, Uwiano wa kimo na uzito, pamoja na kupatiwa ushauri wa kitaalamu kwa wale watakaokutwa na matatizo.

Zoezi hili litafanyika bure na wananchi wote wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma hii muhimu kwa maisha yao.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO