Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Babu wa Loliondo Ajipanga Kwa Ujio Mpya!

Mzee Ambilikile Mwasapile, aliejizolea sifa keme kem kutoka kona zote za Tanzania na nchi jirani kwa alichojipambanua kuwa ni uwezo aliopewa na Mungu wa kutibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia aina fulani ya mti wa porini, anataraji kuja upya na huduma bora zaidi.

Habari zilizopo ni kwamba, Masapila au "Babu wa Loliondo" kama alivyobatizwa na wateja wake, kwasasa anaandaa eneo kubwa takribani ekari saba kwaa ajili ya mapokezi ya wageni watakaojitokeza kutokana na ujio huo mpya.

Haikuweza kufahamika ni lini hasa, Mzee Masapila atarudisha hali ya huduma zake kama alivyoanza mwanzoni. Pamoja na lawama nyingi toka kwa watu ambao walipata "Kikombe cha Babu" bila mafanikio, na wengine kufariki, Mzee Masapila anasema tiba yake inatibu maradhi tu ila haizuii kifo.
Soma zaidi....
Chanzo: Arusha Times
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO