Taarifa za hivi punde kutoka Wilayani Arumeru zinaeleza kuwa aliekuwa Diwani wa Kata ya Nkuarua kupitia CCM, iliyopo katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Bw Emmanuel Wangaeli ameamua kujiuzulu wadhifa huo leo.
Hatua ya kujiuzulu kwake inafuatia mfufulizo wa malalimiko toka kwa wajumbe wa nyumba kumi wa chama hicho katika kata hiyo wakitilia shaka msimamo wake katika maswala mbali mbali ya kisiasa hususani yanayokihusu chama chake.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa, Diwani Emmanuel aliitwa na mabalozi hao jana kwa kikao maalumu lakini alikaidi kuhudhuria kikao hicho, na hatimae leo asubuhi akatoa taarifa ya kujiuzulu kwake.
Aidha, kuna taarifa pia ambazo hazijaweza kuthibitishwa na kiongozi yeyote wa CHADEMA hadi sasa ambazo zinaeleza kuwa mbali na kujiuzulu udiwani, Bw Emmanuel ameamua kukihama chama chake cha awali, CCM na kujiunga na CHADEMA.
arusha255.blogspot.com inaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa hizi na itakujuza kile kilichotokea kwa ukamilifu wake...
2 maoni:
Ukweli hushinda uongo kamanda naamini aliye jiuzulu alikuwa mtiifu kwa ccm akajikuta hana uhuru wa haki
na binadamu ukiwa mtii uka kosa uhuru wewe ni mtumwa
KARIBU CHADEMA TUIKOMBOWE NCHI TUWAPE WANANCHI UHURU WA KWELI NA MABADILIKO YA KWELI

Post a Comment