Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MUAFAKA WA RUGE NA SUGU WAVURUGIKA, MSAKO WA HAKI KUANZA UPYA

sugu Ule muafaka uliofikiwa takribani wiki tatu zilizopita (21 Februari 2012) baina ya Mh Joseph Mbilinyi (Sugu) kama kiongozi wa kundi la VINEGA wanaopigania maslahi stahiki wasanii nchini, na kiongozi wa Clouds Entertainment, Ruge Mutahaba (Ruge), umeingiwa mushkeli na kuna kila dalili ya mparagano kuibuka upya.

Hali hii imejidhihirisha kufuatia taarifa ya Sugu jana kupitia ukurasa wake wa Facebook inayoelezea masikitiko yake kuhusiana na kukiukwa kwa baadhi ya maswala waliyoafikiana hapo awali.

Sugu ndie kiongozi wa VINEGA, kundi la wanaharakati wanopigania haki stahiki kwa wasanii wa muziki nchini, hususani wale wa miondoko ya hip hop na Bongo flava kwa msingi kwamba wamekuwa wakinyonywa kwa muda mrefu.

Hii ni taarifa mpya ya Sugu ikipingana na taarifa ya awali ikihusiha mapatanisho yaliyofanikishwa na Mh Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mh Nchimbi, Waziri wa Vijana Ajira na Michezo.

TAARIFA YA MASIKITIKO

WALIKUJA NA KUOMBA MUAFAKA NASI TUKAKUBALI KWA AJILI YA AMANI NA MAENDELEO YA SANAA,NAMI KAMA KINEGA MWANDAMIZI NA PIA KIONGOZI(MBUNGE) NIKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU YALIYOLETA MACHUNGU YA LAWAMA TOKA KWA MASHABIKI WETU AMBAO KIMSINGI NILIWAELEWA AND I TOOK EVERYTHING AS A MAN...BADO NASIMAMIA KUWA CHOCHOTE NILICHOFANYA NILIAMINI KUWA NILIKUWA NAFANYA KITU POSITIVE, LAKINI KUMBE WENZETU HAWAKUWA NA NIA NJEMA WALA DHAMIRA YA KWELI YA KUTAKA MUAFAKA BALI WALIKUWA NA AJENDA ZAO ZINGINE, MAANA MPAKA LEO HII HAKUNA HATA MOJA WALILOTEKELEZA KUTOKANA NA ULE MUAFAKA, NA ZAIDI MARA WANAKUJA NA HILI LINGINE LA KUWASHTAKI MAPACHA NA HUKU NI WAO WALIOSEMA TUNAANZA 'MWANZO MPYA'...AMBAPO MIMI NILISEMA HAKUNA VITA ISIYOKUWA NA MALENGO NA NILIAMINI KWA DHATI MALENGO YETU SASA YALIKUWA YAMETIMIA...SASA WAO WANAPOJARIBU TENA KUVURUGA UTEKELEZAJI WA MALENGO BASI HAKIKA MALENGO YANAKUWA HAYAJATIMIA NA MAPAMBANO 'INALAZIMIKA' YAENDELEE...

Unaweza pia kujikumbusha pia taarifa ya awali toka kwa Sugu mara tu baada ya muafaka…

“kwanza poleni na samahanini kwa hali ya sintofahamu iliyotokea leo kutokana na taarifa
za ghafla za usuluhishi kati yetu na ruge/clouds fm,ni kutokana na unyeti wa
issue yenyewe ilibidi tufanye hivyo kwa nia njema kabisa...kwanza naomba
tujipongeze kwa kuwa tukio la leo ni ushindi kwa vinega kwa maana kwamba
ma...dai yetu yote ya msingi ndio yalikuwa msingi wa majadiliano na ruge
amekubali kuyatekeleza yote...kuanzia suala la studio ya rais kurudishwa kwa
basata ili iwe ya wasanii wote,pia t.f.u ijikabidhi kwa chama halali cha wasanii
yaani t.u.m.a kama ambavyo tulikuwa tunadai na mpaka issue za wasanii
kunyanyaswa na kubaniwa na pia suala la malipo hafifu vyote vimejadiliwa na
kukubaliwa kwa utekelezaji.

haikuwa kazi rahisi,kwanza ilianza kwa wao kumpigia mwenyekiti wangu mbowe
kutaka tukae chini,ambapo kamanda mbowe alinishauri tukae nao chini kama kweli
wana nia ya kuyamaliza...baadaye wakampigia mr shigongo ambaye ni wazi kuwa ni
kati ya watu wangu wa karibu naye baada ya kuongea na mr. Kusaga tu alinipigia
na kunishauri hivyo hivyo...na kama haikutosha wakalifikisha hili suala kwenye
kamati ya bunge ambayo ilinitaka niipe maelezo ya kiini cha mgogoro na nikafanya
hivyo ambapo pia baada ya kunielewa wakashauri nikae nao chini...na hatimaye
suala hili likaishia mikononi mwa waziri nchimbi pamoja na mhe. Tundu lissu(mp)
kuwa wapatanishi wetu

waziri nchimbi akaanza kwa kumuita ruge dodoma na alikuja tukakaa kwa hatua ya
kwanza na hatimaye leo tukakaa tena makao makuu ya wizara ya utamaduni chini ya
dr nchimbi na mhe tundu lissu na hatimaye tukafikia hatua hii ya leo...vita yetu
ilikuwa na hoja hatukuwa tunapigana tu kwa chuki binafsi kama baadhi ya watu
walivyokuwa wanajaribu kuiweka,kwahiyo kama hoja zetu zimeeleweka kwa sasa
tunatakiwa kushukuru na kufurahi

lakini naomba niwahakikishie misimamo iko pale pale na nimewaweka wazi kuwa
anti-virus itaendelea kuwepo ili kuendelea ku-scan virus wengine kama mameneja
masoko na wengine watakaojitokeza kwani nchi inaposhinda vita au hata kufikia tu
makubaliano ya amani na nchi adui yake haina maana nchi hiyo inavunja jeshi
lake... Asanteni sana”

Gonga hapa kuona mapokeo ya wananchi kuhusiana na taarifa ya muafaka hapo awali..

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO