Hatma ya ubunge wa Godbless Lema (Jimbo la Arusha mjini –CHADEMA) itajulikana Aprili 5 mwaka huu wakati Jaji GabrielRwakibara atakapotoa hukumu ya kesi hiyo ya kupinga matokeo ya ubunge wake.
Kesi hiyo namba 13.2010 iliyofunguliwa na wadai watatu, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agness Mollel, ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Mfawidhi Rwakibalila wa mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Kupangwa kwa siku ya hukumu kunafuatia upande wa walalamikiwa kumaliza kutoa ushahidi wao jana.
Mlalamikiwa wa kwanza katika ksei hiyo, Lema, alikuwa na mashahidi wanne na mlalamikiwa wa pili ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuwa na shahidi yeyote.
Mawakili katika kesi hiyo, Alute Mughwai, anayewatetea wadai na Method Kimongolo anayemtetea mlalamikiwa wa kwanza Lema na Juma Masanja anayemtetea mlalamikiwa wa pili Mwansheria Mkuu wa Serikali, kwa pamoja walikubaliana kuwasilisha hoja za majumuisho kwa njia ya maandishi Machi 30 mwaka huu, kbala au baada ya saa 3:00 asubuhi.
Baada ya makubaliano hayo Jaji Rwakibarila, aliwapangia mawakili hao saa 5:00 kamili ya siku hiyo kuwasilisha hoja za majumuisho ya kisheria kwa njia ya mdomo mahakamani hapo.
Mapema mwaka huu kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, wakili wa wadai Mughwai, alisema angekuwa na mashahidi 25, lakini hadi wanafunga ushahidi ni wau 14 ndio waliokwenda kutoa ushahidi mahakamani hapo.
Hali kadhlalika upande wa mlalamikiwa wa kwanza, Wakili Kimongoro, alisema wangekuwa na mashahidi wasiozidi wanane na Wakili Mwandamizi wa Serikali Timon Vitalis, alisema wangekuwa na mashahidi wawili.
Hata hivyo, baada ya kumaliza shahidi wa nne, Wakili Komongoro aliieleza mahakama kuwa wamefunga ushahidi wao.
Nyongeza na ARUSHA YETU BLOG
Mtu alietajwa na kila shahidi wa upande wa walalamikaji, ambae ndie msingi hoja kuu za malalamiko, Dr Batilda Buriani hakutokea Mahakamani kutoa ushahidi wake.
Chanzo Nipashe, Machi 23, 2012
0 maoni:
Post a Comment