Mamia ya wakazi wa Dar es Slaam na maeneo ya jirani, wengi wakiwa ni wafuasi wa chama cha CUF, leo wamejitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K Nyerere kumlaki Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba akirejea nyumbani toka Marekani alikokuwa kwa zaidi ya miezi 5.
Hivi karibuni, Prof. Lipumba alichaguliwa na jopo la wachumi wa dunia kuwa mwenyekiti wao, nafasi ambayo ameipata kutokana na ujuzi, uzoefu, na elimu aliyonayo katika maswala mambo ya Uchumi.
Akizungumza uwanjani hapo mara baada ya kuwasili, Prof Lipumba alisema kuwa katika mambo aliyotokanayo Marekani ni pamoja na ukweli kwamb uchumi shirikishi na demokrasia, sambamba na utawala bora unaowajibika kwa wananchi ndio nyenzo kuu kwa Bara la Afrika katika kupambana naumasikini.
Alipohitajika kuzungumzia fukuto la migogoro ndani ya chama chake, aliahidi kulitolea majibu swala hilo kesho.
Maandalizi ya mapokezi ya Mwenyekiti huyu wa wachumi Duniani yaliratibiwa kwa sehemu kubwa na chama cha CUF ambapo msafara wake ulielezwa kutakiwa kupita Barabara ya Nyerere, Mandela, Morogoro, Msimbazi, Uhuru, hadi viwanja vya Karume.
Picha: Mjengwa Blog
0 maoni:
Post a Comment