Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DJ Cleo aka Mkali wa " Sizohlangana ku Facebook" Kutoa Burudani Dar es Salaam Leo


Wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani, hususani wapenzi wa miondoko ya kwaito, watapata fursa ya kushuhudia miondoko hiyo live jukwaana toka kwa mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJ Cleo kutoka nchini Afrika ya Kusini anaetamba na wimbo wake wa "Sizohlangana ku Facebook" ambao umejizolea wapenzi wengi hapa nchini.

Mwanamuziki huyo aliewasili jana usiku katika UWanja wa ndege wa Kimataifa JK Nyerere anatazamiwa kufanya maonesho kadhaa nchini. Onyesho lake la kwanza litafanyika leo ukumbi wa Velisa, Kawe, na onesho la pili litafanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam.

kabla ya kuwasili kwake, muandaaji wa ziara ya mwanamuziki huyo nchini, Rehure Nyaulawa alisema kuwa DJ Cleo ataambatana na Dj Soul T pamoja na timu nzima ya madansa wake.

Mwanamuziki huyo mwenye kipaji cha pekee akiwa amejizolea tuzo lukuki kutokana na kazi zake za muzikwa sasa anatamba na nyimbo zake mpya 'Gida' na 'Bhampa Side to Sied' ambazo zinapatikana katika album yake mpya kibisa, Eskhaleni Vol 7&8.

Nyimbo nyingine za msanii huyu zilizojizolea umaarufu ni pamoja na 'Sizohlangana ku Facebook' ambayo ni kama ringtone kwa wapenzi wengi wa miondoko ya kwaito kwasasa nchini, sambamba na nyingine kama 'Ndhamba Nawe', 'Goodbye', 'Mzimba Shaker', na 'Hands Up'.

Mwanamuziki huyu ni wa kipekee kwa maana kwamba hana rekodi ya kufanya vibaya kwenye shoo zake na mara nyingi huwaacha mashabiki wakiwa na shauku ya kuendelea kufurahia burudani yake. Kwa wapenzi wa Afrika Mashariki ambako ni mara yake ya kwanza kutumbuiza wategemee burudani ya kutosha.

Katika ziara yake hiyo nchini atasandikizwa na wasanii wa nyumbni hapa kama Suma Lee "Mzee wa Hakunaga", Ommy Dimpoz, Dully Sykes, Chege&Temba, Tip Top Connection na Linex kwa kutaja wachache.

Picha: kwa hisani ya FULLSHANGWE BLOG
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO