Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Akanusha Kuongezwa Vituo Hewa Arumeru Mashariki

1 Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC)Jaji Mkuu mstaafu Bw. Damiani Lubuva akiongea na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo jijini Dar es salaam, kuhusiana na uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru mashariki kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi huo, ambapo Jaji Lubuva amekanusha vikali tuhuma za kuongeza vituo bandia zilizotolewa na chama cha (CHADEMA)

Katika picha kulia Mkurugenzi wa tume ya uchakuzi Bw. Julias Mallaba, Kushoto Jaji mkuu mstaafu Zanzibar Makamu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw. Hamio Mahmoud Hamio.


Hatua hii inafuatia tuhuma zilizotolewa jana na Dr Slaa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokraisa na Maendeleo, CHADEMA kuwa ana taarifa za kuwako vituo hewa 55 katika Jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili 1, 2012 ili kumpata Mbunge mpya kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliekuwa Mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremia Sumari. Jumla ya vyama 8 vinashiriki uchaguzi huo na machuano mkali uko baina ya CCM na CHADEMA.

Picha: FULL SHANGWE

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO