Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ARUMERU LEO: CCM WAMTEKA MWENYEKITI WA CHADEMA

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi wamekamata Mwenyekiti wa Tawi la CHADEMA  Magadirisho leo, na kumpeleka msituni ambapo walimpiga sana na kumbana sehemu za siri ili aseme ni akina nani waliwapiga CCM jana maeneo ya Maji ya Chai. Baadaye walimpeleka polisi akiwa hoi! Lakini baada ya kuhojiwa na polisi waligundua hana hatia.

Akizungumzia tukio hili kwa masikitiko makubwa, Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Taifa, Ndg John Heche alisema kitendo walichofanya CCM hakivumiliki, na hakitakubalika.  “Tutakua wapole lakini hatutakua wanyonge, kitendo walichofanya viongozi wa ccm kumteka mwenyekiti wetu wa tawi la Magadirisho kumpiga na kumminya sehemu zake za siri hakikubaliki na hatutakivumilia” alieleza

Itakumbukwa kuwa katika uchaguzi mdogo kule Igunga Oktoba mwaka jana, CCM walikumbwa na kashfa ya kuteka vijana wa CHADEMA wanaotokea kwenye mikutano yao hasa wakati inapotokea kuonesha hisia zao tofauti na uhitaji wa CCM. Kuna wakati vijana kadhaa walitekwa mbele ya Mh Wassira akiwa anahutubia, na wakatokomea nao kusikojulikana.

Kumbukumbu ya kusikitisha zaidi kule Igunga, mbali na tukio la mwanaCCM kumwagiwa tindikali, ni ile ya kijana mwanachama wa CHADEMA Mbwana Masoud kukutwa amerafiki baada ya kukosekana kwa muda wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga. Marehemu Mbwana Masoud alikuwa ni mmoja wa wanachama walijitolea kusafiri toka Dar es Salaam kwenda Igunga kwa ajili ya kuwa wakala kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 2 Oktoba 2011.

Kwa mujibu wa kumbukumbu Marehemu Mbwana Masoud alitoweka katika mazingira ya kutatanisha wilayani Igunga tarehe 2 Oktoba 2011.Baada ya jitihada za viongozi wa chama kumtafuta marehemu kushindikana Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika (Mb) alitoa taarifa polisi tarehe 3 Oktoba 2011 na kufungua jalada RB/748/2011.

Tarehe 9 Oktoba 2011 wananchi wilayani Igunga walikuta mwili wa marehemu ukiwa porini katika eneo ambalo linajulikana zaidi kama msitu wa magereza.Taarifa ilitolewa na wananchi kwa diwani wa kata ya Igunga Vicent Kamanga (CHADEMA) ambaye alifika katika eneo hilo na baadaye maafisa wa polisi walifika na kupeleka mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Kutokana na hali ya mwili wa marehemu kuharibika sana, maziko yalifanyika tarehe 11 Oktoba 2011 alasiri katika kata ya Igunga yakihusisha wawakilishi wa familia ya marehemu, viongozi wa chama, wanachama na wananchi wa Igunga.

Hii ni rekodi mbaya, na haipaswi kujirudia kwasababu siasa sio vurugu. Matukio kama haya ya utekaji yakiachiwa kuendela kutendeka nchini, amani ya taifa hili itakuwa mashakani na ni vigumu sana kuirudisha pindi ikitoweka..

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO