Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

LATEST NEWS: KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MGOMO WA MADAKTARI IKULU, AAHIRISHA KUKUTANA NA WAZEE WA DAR HADI JUMATATU JIONI


Rais Jakaya Kikwete, amefanya kikao cha ghafla na uongozi wa madaktari ambao wameanza mgomo wao upya wakidai maslahi zaidi na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi ili kutoa huduma bora.

Rais Kikwete ambaye leo alikuwa akutane na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam sasa atakutana na wazee Jumatatu, Machi 12, 2012 saa kumi jioni, katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Awali iliahirishwa hadi kesho saa tano asubuhi lakini ikaonekana iwe Jumatatu ili Rais aweze kupata mashauriano kuhusu swala alilopanga kueleza.

Ilielezwa kwamba mkutano wa wazee na Rais umeahirishwa ili kutoa nafasi kwa Rais kufanya mashauriano zaidi na wadau mbali mbali kuhusu suala ambalo Rais atalizungumzia kwenye mkutano huo.

Kama ulivyokuwa mkutano ulioahirishwa leo, mkutano wa kesho utafanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa tano asubuhi.

Chanzo: TBC na FikraPevu.Com
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO