Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TBC yalaumiwa kuripoti kampeni upande mmoja Arumeru Mashariki

tbc Kwa siku takribani mbili sasa kumekuwepo na mfululizo wa malalmiko miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuhusiana na namna ambavyo Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limekuwa likiripoti matukio ya kampeni za Uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha.

Katika malaliko yao, wanaeleza kuwa chombo hiki cha habari kimewanyima fursa ya kuweza kujua kile kinachoendelea Arumeru kwa uhalisia wake. Wakitolea mfano, wanadai kwa takribani siku nne mfululizo wamekuwa wakifuatilia matangazo ya kituo hicho lakini wakaishia kukutana na matangazo na mwenendo wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi, CCM pekee. katika taariza zao za habari.

Kwa jinsi mjadala ulivyokuwa hawakuridhishwa na hali hiyo kutokana na ukweli kwamba taarifa za awali zinaeleza kule Arumeru kuna jumla ya vyama 8 vinavyoshiriki uchaguzi na vyote vinastahili kupatiwa nafasi ya habari zao kusikika kwenye kituo hiki cha umma kwasababu kinaendeshwa kwa kodi za watanzania wote, na hata wasio na itikadi za kisiasa.

Walidai TBC kutoonesha kampeni za vyama vingine ni kutowatendea haki watanzania, na haipaswi kuegemea upande wowote katika kuripoti habari zake kama miiko ya taaluma ya habari inavyoeleza.

Hata hivyo, uchunguzi wa arusha255.blogspot.com umegundua kuwa, mshawasha wa wananchi hao kutaka kuona habari za vyama vingine unatokana na ripoti za vyombo vingine vya habari nchini hususani magazeti huru yakiripoti upinzani mkali toka vyama vingine, hususani Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA dhidi ya chama tawala CCM.

Mjadala huo haukuweza kupata hitimisho lakini uliishia kwa kujiuliza, je vyama vingine vilivyopo Arumeru katika kampeni havistahili kupata fursa hiyo ukizingatia kuwa TBC ni chombo cha umaa na kinachoendeshwa kwa kodi za watanzania wote bila kujali dini, rangi, kabila na itikadi za kisiasa?

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO