CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kinatarajia kuzindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki kesho Jumamosi Machi 10.
Akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kwa Marafiki wa CHADEMA Arusha iliyofanyika katika Hoteli ya kitalii ya Kibo Palace juzi, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema kwamba wanatarajia kuzindua kampeni za chama hicho kesho Jumamosi katika eneo la Usa River, kamapeni ambazo zitasimamiwa na Mbunge wa Musoma Mjini, Mh Vicent Nyerere.
Alisema kikosi kizima kwa jili ya kampeni kiko tayari mjini Arusha na kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuhudhuria mikutano ya chama hicho ili kuweza kujua dhamira ya chama katika kumkomboa mtanzania. Alidai chama hicho hakitaota magari ya kuwasafirisha watu kwenda kwenye mikutano kwa kuwa sio utamaduni wake.
Akitoa salamu zake wakati wa hafla hiyo, Mbowe aliwakumbusha wanachama wa chama hicho ambao wanadhani wako ndani ya chama hicho kwa ajili ya kuvuna kwa faisda ya mfumo wa vyama vingi, wajione hawako mahali sahihi. Aliongeza kuwa CHADEMA kama chama cha siasa kinapaswa kusimamia dhamira yake ya kweli kama chama kilichodhamiria kuwakomboa watanzania.
Akitumia mfano wa Mwalimu Nyerere, aliewahi kukiri kuwa CCM si mama wala baba yake, basi na mwanaCHADEMA yeyote anapaswa kusimamia hilo pia, kwamba CHADEMA isiwe mama ama baba ya mwanachama. Kila mwanachama ajitahiki kukisaidia chama kisimame katika misingi yake na pindi kikienda kinyume awe huru kukuacha.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti huyo alisema CHADEMA inataka kutumia uchaguzi mgodo wa Arumeru Mashariki ili kuweza kuwafikishia ujumbe watanzania kuwa fedha sio kitu katika kupigania haki yao. Alisema kuwa CHADEMA inatarajia kutumia bajeti ndogo katika uchaguzi huo na sehemu kubwa itatokana na nguvu ya wananchi.
Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, maalumu kwa Marafiki wa CHADEMA (Justice of CHADEMA) kufahamiana na kuwafahamu viongozi wa chama hususani ngazi ya mkoa, mbali na Mh. Mbowe, walikuwepo pia viongozi wa chama hicho kama Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema, Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha, Ndg Samson Mwigamba, Katibu wa CHADEMA Arusha, Ndg Amani Golugwa, na Mwenyekiti wa Vijana wa chama hicho Arusha, Ndg Ephata Nanyaro.
Wengine ni Katibu wa vijana wa CHADEMA Arusha, Mss Julysiza Mengiseni, Mgombea wa chama hicho Arumeru Mashariki Ndg. Joshua Nassari, pamoja na Diwani wa Arusha mjini viti maalumu kupitia chama hicho.
Taarifa zaidi kutoka kwa Mkurugenzi wa Bunge wa CHADEMA, Bw. John Mrema, amekaririwa akisema kabla kuwa ya uzinduzi, Mwenyekiti huyo anatarajiwa kupokewa kwa maandamano makubwa.
Katika hatua nyingine, inaelezwa kuwa hapo awali, vyama vya CHADEMA na CCM vilikuwa vizindue kampeni zao siku moja ya Jumamosi. CCM walipanga kuwa eneo la Tengeru Sokoni na CHADEMA eneo hilo la Usa River, maeneo yanapopishana kwa takribani km 1 tu, lakini taarifa za sasa ni kuwa CCM wameahirisha uzinduzi wao hadi Jumatatu Machi 12.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment