Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WANAJESHI WAASI WAIPINDUA SERIKALI YA MALI

BamakoWanajeshi waasi wametangaza katika televisheni ya taifa ya Mali kuwa wamechukua udhibiti wa nchi, saa kadha baada ya kuvamia kasri ya rais.

Wanajeshi walioasi wanasema kuna marufuku ya kutotoka nje katika nchi nzima na kwamba katiba haitatumika kwa sasa.

Siku ya Jumatano wanajeshi hao walifyatuliana risasi na wanajeshi watiifu kwa serikali.

Wanasema serikali haijawapa silaha za kutosha kukabiliana na waasi wa jamii ya Tuareg.

Tayari walikuwa wamechukua udhibiti wa kituo cha taifa cha redio na televisheni na kusitisha matangazo.

Baada ya saa kadha ya kuonyesha picha za nyimbo za wanamuziki wa Mali, kundi la wanajeshi likaonekana kwenye televisheni mapema siku ya Alhamisi, wakitambulishwa kama "Kamati itakayorudisha Demokrasia na kutuliza hali katika nchi".

Msemaji wa waasi hao, aliyetajwa kwa jina la Luteni Amadou Konare, alisema sasa wamemaliza "utawala usio thabiti" wa Rais Amadou Toumani Toure

Chanzo: BBC

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO