UJUMBE wa chama cha African National Congress (ANC), kutoka Afrika Kusini unatarajiwa kushiriki kongamano lwa wafanyabiashara litakalofanyika kesho Jumanne Machi 27, 2012 Jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo limeandaliwa na Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Hamashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye, watendaji wa Chama Cha Mapinduzi watashiriki kongamano hilo pia, lengo likiwa ni kujifunza mbinu za biashara.
Itakumbukwa kwamba chama cha ANC kina historia ndefu sana na Tanzania. Kwa mfano, mkutano Mkuu wa kwanza wa chama hicho ulifanyika mkoani Morogoro, kuanzia 25 Aprili hadi 1 May 1969.
Mkutano huo ulihudhuriwa na zaidi ya wajumbe sabini kutoka matawi tofauti ya chama hicho kwa wakati ule na baadhi ya wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa Bw. A Swai, aliekuwa Katibu Mtendaji wa Mambo ya Nje TANU,
na Bw. J J Nambuta wa NUTA, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanganyika.
Wengine ni Bw Amadou N`diaye, aliekuwa Katibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Afrika kiongozi wa kimapinduzi wa FRELIMO (Msumbiji), vyama vya MPLA (Angola), SWAPO (Namibia) na ZAPU (Zimbabwe).
0 maoni:
Post a Comment