Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Mh Godbless Lema amekanyaga ardhi ya Arumeru leo kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za chama chake ambapo leo ilikuwa ni siku ya Uzinduzi Rasmi wa kampenzi za kumnadi mgombea wa chama hicho, kijana Joshua Nassari.
Kampeni hizo ni kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki unatorajiwa kufanyika Aprili mosi mwaka huu, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, marehemu Jeremia Sumari aliefariki Januari 19 kutokana na matatizo ya kansa ya ubongo.
Mh Lema akiwa miongoni mwa viongozi na wabunge wa CHADEMA waliohudhuria uzinduzi huo uliofanywa na Mwenyekiti wa chama hicho, ambae pia ni Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe, katika viwanja vya shule ya msingi Liganga, Usa River, alishangiliwa sana na maelfu ya watu waliohudhuria uwanjani hapo mara alipotajwa kuwasalimia.
Kitendo cha Lema kuingia Arumeru kwa shughuli za kisiasa ilihali kuna uvumi kuwa hatakiwi kuingia Wilayani humo, kiliweza kufuta vichwani mwa watu, taarifa za awali kwamba wazee wa Kishiri Wilayani Arumeru wamempiga marufuku kuingia huko na kama akikaidi watamuua, taarifa ambazo zilipata kuzungumzwa pia na Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Bw John Tendwa. Kwa ujumla hakukuwa na dalili yeyote ya kutokea madhara kwa Mh Lema pamoja na kwamba alifika mapema sana viwanjani hapo.
Akizungumza katika mkutano huo mara baada ya kupewa nafasi kuwasalimia wananchi, huku akishangiliwa sana, Lema alianza kwa kuuliza alipo ndugu wa mgombea wa chama kingine ambae aliewahi kaririwa akieleza kuwa Lema amepigwa marufuku na Wazee wa Arumeru kutokanyaga ardhi ya Arumeru.
Akiongea kwa kujiamini, Mh Lema aliwaahidi wananchi wa Arumeru kuwa atakuwa nao pamoja kuanzia wiki ijayo. Akasema kuwa atalala Arumeru kwa muda wote atakaokuwepo Wilayani humo akifanya kamapeni za kumnadi Joshua Nassari.
Aidha, katika hatua ambayo Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw Mbowe alieleza ni uamuzi wa kukirudisha chama kwa wananchi na kwamba kwa kuanzia, gaharama za kugharamia uchaguzi wa Arumeru Mashariki zitatoka kwa watanzania, Mh Lema alibeba jukumu la kupitisha ‘bakuli’ kwa awamu ya pili kkusanya mchango wa Mbunge, akiwa ameongozana na mgombea Joshua Nassari.
Uamuzi wa Lema kutaka kuzunguka kwa wananchi na ‘bakuli’ nje ya njia iliyoandaliwa ulitaka kupingwa na askari waliokuwepo kuhakikisha usalama wa kila raia, lakini kwa maombi binafsi, Lema alikataa kupita kwenye njia iliyaoandaliwa kiusalama na badala yake akaingia katikati ya wananchi ambako aliweza kukusanya pesa pamoja na kuzongwazongwa sana hali iliyowaongezea kazi askari wachache waliokuwa wanamlinda katikati ya umati wa watu.
Awamu hii ya uchagishaji ilifuatia, awamu ya kwanza iliyotangazwa na Mh Mbowe na kusimamiwa na vijana wa Red Briged ya chama hicho, sambamba na namba za simu kwa ambao walikuwa mbali na pale uwanjani lakini walikuwa wanafuatilia mkutano mojakwamoja kupitia televisheni na redio. Mh Mbowe alitangaza namba hizo kuwa ni M-PESA 0757 755 333, tiGO Pesa 0655 783 333 na Airtel Money na zitatumika hadi mwisho wa Uchaguzi, na hivyo kuwataka watanzania popote pale walipo wachangie kile walichonancho ili kuwa sehemu ya mabadiliko.
0 maoni:
Post a Comment