Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UCHAGUZI ARUMERU: CCM Wagawa Nakala Za Gazeti Bure Mikutanoni Kuwachafua CHADEMA

DSCN9958

Taswira ya Gazeti SAUTI HURU ukurasa wa mbele, toleo Na 177 la Machi 23 –27, 2012 lililogawiwa bure na maofisa wa CCM kwa watu waliohudhuria mikutano yao King’ori, Patandi, Legaruki na Maji ya Chai

the arusha report inaweza kuthibitisha..

Mamia ya nakala za gazeti la kila wiki, SAUTI HURU (pichani juu) ambalo hutolewa na kampuni ya Free Voice Investments  ya Kariakoo- Jijini  Dar es Slaam juzi zilikuwa zikigawiwa bure kwa watu waliofika kwenye mikutano ya kampeni za mgombea wa CCM, Sioi Sumari.

Gazeti hilo liligawanywa bure na maofisa wa CCM kwa wananchi waliofika kwenye mikutano ya King’ori, Patandi – Maji ya Chai na Leguruki.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za kufanya hivyo, lakini kwa maudhui ya kilichonadikwa na kusimuliwa ndani ya gazeti hilo ni rahisi kuamini usambazaji huo na ugawaji bure wa gazeti hilo unalenga kuwatisha watu na pia kuwachafua CHADEMA.

Wazo hilo linaungwa mkono na Mratibu Mkuu wa Operesheni wa Kampeni wa Chadema jimboni Arumeru Mashariki, John Mrema ambae alisema ni dhahiri kwamba gazeti hilo linasambazwa kukichafua chama hicho na kwamba bado wanatafakari hatua za kuchukua.

DSCN9959

Moja ya kurasa za ndani ikiwa na picha za matukio tofauti ya kampeni ya mgombea wa CCM, jambo ambalo linaweza kuonesha kuwa CCM inatumia gazeti hilo na taarifa zilizochapwa na kusambazwa zilifanyika kwa uelewa wa CCM, pengine kwa maagizo yao.

Gazeti hilo toleo nambari 177 la Machi 21 – 27, 2012 lina taarifa nyingi zinazohusu uchaguzi wa Arumeru zikilenga kupotosha uhalisia wa mambo Jimboni humo kwa kuandika propaganda za kuwachafua CHADEMA ambao wametokea kuvutia na kuungwa mkono na watu wengi sana katika mikutano yao mijini na vijijini tofauti na ilivyo kwa upande wa CCM.

Habari kuu iliyojiuza ukurasa wa mbele wa Gazeti hilo inasema “CHADEMA wakata tamaa” na kufuatiwa na vichwa vidogo vya habari..“Mbowe adaiwa kukiuza (CHADEMA) na kuingia mitini’, “Mungiki kuanza kazi rasmi muda wowote”, “Meseji za Nassari zanaswa akikiri kushindwa”, “Chadema waburuzana kortini..wenye elimu ndogo waitwa virusi…watakiwa kuondoka ndani ya chama”

Tahariri ya Gazeti hilo, ipo uk wa 4 na imepewa kichwa cha habari “CHADEMA iache kufanya uhuni Arumeru”

Maelezo ya Mhariri wa gazeti hilo, ndani ya tahariri hiyo yanapandikiza chuki ambayo haipo na kutisha wananchi kwamba CHADEMA imeandaa vijana wake maarufu kama Mungiki kuanza kuwapiga watu ili kuwatia hofu hasa wazee na kina mama wasije kujitokeza kupiga kura ili vijana wachache wasiohofia kitu ndio wajitokeze kupiga kura.

Tahariri inaongezea zaidi “Ni heri ukutane na nyuki wenye hasira kuliko kukutana na Mungiki wa CHADEMA. Asiyefahamu hilo anaweza kumuuliza DC wa Igunga aliyejikuta akivuliwa NGUO hadharani mbele ya vijana wababe na watiifu kwa Freeman Mbowe”

Akihitimisha tahadhari ya kukutana na anaowatambulisha kama Mungiki wa CHADEMA Mhariri anamaliza kwa kusema “Hata hivyo hatutegemei kuwa hili ni jeshi linaloweza kushindana na jeshi la Polisi bali ni mkusanyiko wa WAHUNI tu wa kawaida wanaofanya kazi hiyo kwa ujira mdogo tena wakati mwingine kwa mkopo usio na uhakika wa kulipwa”

Ukurasa wa mbele wa gazeti hilo, wamechapisha picha ya Mbowe kushoto na kulia ya kijana aliemwagiwa tindikali kule Igunga ikiwa na maelezo “Mmoja wa Vijana waliokutana na tindikali ya Mungiki wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Igunga mwishoni mwa mwaka jana”

Inafahamika wazi kuwa hili la kumwagiwa tindikali Igunga mwaka jana, ni swala ambalo jeshi la Polisi lilibeba jukumu la kuwasaka na kuwakamata wahusika wa tukio lile ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, ili ijulikane ni watu walikuwa wametumwa na CHDAEMA ama vinginevyo. 

Lakini mpaka leo hii, watu hao hawajaweza kufahamika, wacha kuthibitishwa uhusika wa CHADEMA, jambo ambalo linaweza kusadifu mawazo ya wanaoamini kuwa ulikuwa ni mchezo walioufanya wenyewe CCM kwa malengo waliyoyajua wenyewe!

Kwa kipindi kirefu sasa, CCM wamekuwa na desturi ya kulazimisha kampenzi za wapinzani wao zionekane ni vurugu na kuwalazimisha wananchi waamini kuwa watu wa upande wa upinzani ni makatili, wauaji na watu hatari katika nchi. Haya ymeshuhudiwa Igunga, Musoma, Busanda na kungineko ambako kumekuwa na chaguzi ndogo za ubunge ama udiwani.

Na jambo la kusikitisha zaidi, tuhuma hizi zinaashiria hatari kwa usalama wa nchi na watu wake wakati sio kweli, lakini vyombo vya usalama vimeshindwa kukemea hali hiyo. Unaweza kujiuliza, kama kweli kuna kundi hatari la kudhuru watu liko nchini na linafahamika, imeshindikana vipi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili watu hao wakadhibitiwa ili wasilete madhara!?DSCN9962

Hii ndio habari inayolalamikiwa kutungwa kuwachafua CHADEMA

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la jana, Mhariri wa gazeti la Sauti Huru alipoulizwa kuhusiana na kusambazwa huko bure lisema: "Sifahamu chochote kuhusu suala hilo, labda CCM wamenunua nakala nyingi kwa ajili ya kuwagawia watu wao lakini ngoja nifuatilie maana sikuwapo ofisini kwa wiki nzima".

Aidha itakumbukwa kwamba Mungiki ni kundi la kisiasa-dini na ni shirika la kihalifu lililopigwa marufuku nchini Kenya. Jina hile linamaana ya "umoja wa watu" au "umati" katika lugha ya Kikuyu. Dini hii, ambayo aghalabu ilianza katika miaka ya 1980, ni ya kisiri na hukuza ulinganishi na dini mafumbo. Haswa asili yao na mafundisho yao haielewiki.

Kilicho wazi ni kwamba Mungiki hupendekeza kurudi kwa desturi za Kiafrika kama vile kulazimisha tohara ya wanawake.wao hupinga mila za kizungu na mambo yote ambayo wao wanaamini kuwa mitengo ya ukoloni ikiwemo ukisto. Itikadi ya kundi hili inahusisha mapinduzi ya kughulumisha,mila za kikuyu,uvunjifu wa sisasa wa Kenya, ambao kuonekana kama wazinzi rushwa. Mungiki mara nyingi hujulikana kama Kenya's Cosa Nostra, Yakuza, au Mafia Kenya kutokana na ushirika wake.

Kwa hiyo utaona Mhariri kutumia neno “Mungiki wa CHADEMA” ni kutaka kuwatia hofu wananchi na kupandikiza chuki ambayo athari zake zinaweza kuwa mbaya sana.

Hata hivyo, ni bahati nzuri kwamba propaganda hizi zinakuja kipindi na katika mazingira ambayo wananchi wengi ni waelewa, na hakuna matukio yaliyoripotiwa na Jeshi la Polisi kuhusu uwepo wa kikundi cha uhalifu Jimboni humo, na kwa ujumla wake kampeni za Arumeru zimekuwa za amani muda wote tangu kuanza kwake kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo ukiacha rabsha ndogo ndogo za kuzomeana, tofauti na ilivyokuwa kwa matukio ya kuumizana na hadi kuuana kule Igunga, mwishoni mwa mwaka jana.

Matukio makubwa kuripotiwa na kuthibitishwa kutokea Arumeru, ni kuhusiana na kurushiwa mawe kwa msafara wa waandishi wa habari wa CCM kulikohisiwa kufanywa na wafuasi wa CHADEMA, na lile la mwenyekiti wa Tawi la CHADEMA kutekwa na kupelekwa msituni alikoteswa na kubinywa mapumbu ili ataje ni viongozi gani wa CHADEMA waliogiza msafara huo urushiwe mawe, swala ambalo lilifanyika kama kulipiza kisasi kwa kuhisi tu.

Pamoja na mwenyekiti huyo kupelekwa Polisi kama mtuhumiwa, bado haikuweza kuthibitika kama ni wafuasi wa chadema ndio walihusika, na kiongozi huyo aliishia kupata mateso ambayo hayakumstahili katika tukio ambalo lililaniwa vikali na viongozi wa CHADEMA na wapenda haki na amani jimboni humo.

*Hapo ndipo siasa za chama kikongwe nchini zilipofikia*

The Arusha Report

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Anonymous said...

soon tutaona CCM wakichanganyikiwa, haiwezekani mtu atoke na kusema uongo tena kwa kulazimisha watu wasome halafu tuseme ana akili timamu, Go go go go CDM

Anonymous said...

ni mamabo ya ajabu kidogo kufanyika katika karne hii ya sasa ambayo watu ni waerevu... inawezekana kitengo cha propaganda bado kina mbinu za kizamani sana, tena ni mbinu za kigaidi maana wako tayari kumtoa kafara mwenzao ili maneno watakayoyasema yaendane na tukio..

kwa mfano hivi sasa wanatumia hata misiba, mtu ambae amejifia kwa taratibu na mapenzi ya Mungu wao wanaanza kuwatupia lawama wapinzani wao kuwa wamemuua!!

lakini hii inanikumbusha wakati vyama vingi vinaanza nchini ambapo wananchi walikuwa wanawekewa mikanda ya mauaji ya kimbari huko Rwanda ili watishike wasiweze kuiwajibisha serikali, huku wao wakiendelea kutafuna mali za taifa...

hapa unapata kujiuliza jamabo moja tu, kama hawako tayari kuona uchaguzi unakuwa huru na wananchi wanajichagulia kiongozi wanaempenda, kwanini wanatangaza uchaguzi!?

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO