SIASA chafu za kupakana matope zimeanza kujitokeza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ikiwa ni wiki moja tu tangu kuanza kwake.
Miongoni mwa malalamiko yanayotolewa ni kusambazwa kwa nyaraka za kashfa, wafuasi kufanya fujo katika mikutano ya vyama pinzani, watu kuzuiwa kushiriki kwenye mikutano ya kampeni, matumizi ya lugha chafu dhidi ya viongozi wakuu wa vyama pinzani kwenye majukwaa ya kampeni na kusambazwa kwa taarifa za uchochezi zinazowashawishi wananchi wasishiriki kampeni. Read more...
Published by Mwananchi Habari on 17th March, 2012
0 maoni:
Post a Comment