Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UZINDUZI WA KAMPENI (CHADEMA): PICHA ZA MATUKIO KABLA YA HOTUBA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimezindua kampeni zake leo kwa uchaguzi wa Arumeru Mashariki unaotarajiwa kufanyika April mosi. Uzinduzi rasmi kulianza saa9:00 jioni, katika uwanja wa shule ya Msingi Liganga, Usa River, Arumeru na kurushwa moja kwa moja na kituo cha Star Tv pamoja na Sunrise Redio ya Arusha.
Baadhi ya picha za matukio ya awali kabla ya uzinduzi, miongoni mwake ni hizi hapa…

DSCN9981Jukwaa kuku lilivyoandaliwa

 

DSCN9983Baadhi ya viongozi wa dini wakiwasili na kuelekea sehemu waliyopangiwa

DSCN9994 Njia ya kuingia Jukwaa kuu.. Pembeni wanakaa wanausalama wa CHADEMA

DSCN9974Ilikuwa ni mwendo wa kuserebuka wakati viongozi wanasubiriwa

DSCN9958Kutoka kushoto; Zitto Kabwe, Mch Msigwa, na Gobless Lema. Hapa Lema hakuwa katika gwanda la shughuli rasmi…alibadilika baadae

DSCN9969 Zitto Kabwe akiteta jambo na wanausalama, John Mrema anaonekana akitabasamu

DSCN9942 Mh Joseph Mbilinyi aka Sugu aliwahi mapema jukwaani

DSCN9928Shamrashamra barabarani kuelekea uwanjani

DSCN9949  Jukwaa la viongozi mbalimbali wa CHADEMA

DSCN9950Viongozi wa CHADEMA Mkoa; Ephata Nanyaro, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa akiwa bize na kilongalonga

 

DSCN9992   Mchungaji Natse, Mbunge wa Karatu akiteta jambo na Sheikh Sadik aliefanya swala ya kufungua mkutano

DSCN9930Biashara nazo hazikukosekana



Buraudani ya Farasi ilikuwepo wakati viongozi wanasubiriwa
Kijua cha saa saba kilikuwa kikali hadi kulazimu raia kujificha chini ya miti iliyopo uwanjani hapo wakiwasubiri viongozi..
Hapa ni wataalamu wa kurusha matatngazo ya mojakwamoja wakiwa wanaseti vifaa vya kazi..
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO