Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa idadi ya wapiga kura walioandikishwa kushiriki katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki imeongezeka hadi kufikia 127,455, ikiwa ni ongezeko la watu 26 kutoka watu 127,429 waliokuwepo kwenye orodha iliyotumika mwaka 2010.
Akiongea na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alisema ongezeko hilo la watu 26 limegundulika wakati Tume yake ikifanya mapitio na kurekebisha kasoro katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura.
Alisema, watu hao 26 walikuwa wameandikishwa kwenye daftari la wapiga kura lakini majina yao hayakuonekana kwenye orodha ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Akifafanua zaidi Jaji Lubuva alisema, kimsingi waligundua karoso zilizokuwa zinawahusu takribani wapiga kura 58 katika uchaguzi uliopita. Kati ya hao, 28 ni waliokuwa wamejiandikisha zaidi ya mara moja, na waliobaki (26) ni wale ambao majina yao hayakuonekana katika uchaguzi wa 2010.
Aidha jaji Lubuva alisema kuwa hakuna jina la mpiga kura jipya lililoongezwa, na hakuna jina la mpiga kura mpya lililoongezwa.
Wakati akitangaza hayo, alitumia fursa hiyo pia kukanusha tuhuma za Tume yake kuongeza vituo bandia 55 kinyemela. Alisema idadi ya vituo 327 iliyokuwepo uchaguzi ulipita ndiyo itakayotumika.
Awali kulikuwa na tuhuma kuwa kuna vituo 55 vipya vimeongezwa bila taarifa na kufikia vituo 382. Tuhuma hizi zilitolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa akieleza kukamata nyaraka za siri zinazoonesha ongezeko la vituo hivyo alivyodai kuwa bandia, tuhuma ambazo alizirudia tena kwenye mikutano ya kampeni za chama chake Jimboni humo jana.
Chanzo: The Citizen
0 maoni:
Post a Comment