News Alert: Uzinduzi wa Kampeni Za CHADEMA Kurushwa Live Star Tv
CHADEMA wanatarajia kuzindua rasmi kampeni kwa ajili ya uchaguzi mgogo Jimbo la Arumeru Mashariki leo Jumamosi Machi 10, uzinduzi unaoelezwa utatanguliwa na maandamano ya amani.
Katika sherehe za uzinduzi huo zitakaofanyika eneo la Usa River, Mh Freeman Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atalihutubia taifa kupitia televisheni na redio.
Arusha255 inaweza kuthibitisha kuwa, kwa mujibu wa maandalizi rasmi ya ufunguzi, hotuba hiyo ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA utarushwa mojakwa moja kutoka Uwanja wa Shule ya Msingi Liganga, Usa River, kupitia Star Tv ya Mwanza, Redio Sunrise FM ya Arusha na Redio MJ FM ya Arusha pia, kuanzia saa 9:00 alasiri.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Tanzania,watanzania wataweza kushuhudia kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge. Mara nyingi imezoeleka kuona uzinduzi wa chaguzi kuu hususani kwa ngazi ya urais zikirushwa hewani mojakwamoja siku ya ufunguzi.
Jumla ya wapigakura 127,000 waliojiandikisha katika daftari liliotumika Uchaguzi Mkuu uliopita ndio wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi huu mdogo, kwa jumla ya vituo 327 vya kupigia kura. Vyama vinane vinashiriki uchaguzi huu wakiwemo CHADEMA, CCM, NRA, TLP, UPDP na SAU.
0 maoni:
Post a Comment