Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Alert: Kikwete Kuzungumza na Wazee wa Dar Kesho Jioni!

Kuna taarifa zisizo ramsi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya M Kikwete anataraji kuongea na 'wazee wa Dar es Salaam" kuhusiana na maswala ambayo hayakubainishwa kesho jioni(Ijumaa 09/03/2012).

Kama ambavyo iliwahi kutokea tishio la mgomo wa wafanyakazi, na Rais kujitokeza kuongea nao kwa ukali sana, kwa mgomo huu wa madaktari unaoendelea nchini hivi sasa hali ni tofauti. Busara ya hali ya juu inahitajika ili kuweza kumaliza tatizo. Haijaweza kufahamika mara moja ni nini hasa Rais anataka kuzungumza na kwanini iwe ni mazungumzo na wazee wa Dar.

Ni swala la muda, na subira huvuta heri kama wasemavyo waswahili!
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO