CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilianza kutumia helkopta rasmi katika kampeni zake za kumnadi mgombea wake wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassa.
Mara ya mwisho kutumia chombo hicho ilkuwa ni Machi 10 wakati wa ufunguzi wa kampeni.
Mkuu wa Operesheni wa uchaguzi wa Chadema katika jimbo hilo, John Mrema anasema kuanza kutumika kwa helkopta hiyo kutamwezesha mgombea wao kufanya mikutano mitano hadi nane kwenye kata tano tofauti kwa siku.
Mikutano ya jana ilifanyika katika vijiji vya Ngurdoto Kata ya Maji ya Chai, Ngabobo Kata ya Ngarenanyuki, Kijiji cha Sakila Kata ya Kikatiti na vijiji na kata za King’ori na Nkoanrua.
Katika mkutano wa Kata ya Ngarenanyuki, mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari alichinjiwa ng’ombe wanne na kuvalishwa mgolole sambamba na kukabidhiwa rungu la Kimasai.
Mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari akisalimia wananchi mara baada ya kuwasili uwanjani kati ya moja ya mikutano yake jirani na Sing’isi
Dr Slaa akimnadi mgombea wa chama chake
Karibia kampeni zote, CHADEMA wamekuwa wakitumia magari yao mawili maalumu kwa matangzao ambayoyana jukwaa na PA System, Generator na kila kitu hapo hapo.
0 maoni:
Post a Comment