Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWAKYEMBE AREJEA JANA TOKA INDIA, KUINGIA OFISINI JUMATATU

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amerejea nchini akitokea India alikokwenda kwa matibabu na kueleza kuwa atazungumzia, pamoja na mambo mengine, afya yake keshokutwa atakapoingia ofisini.


Hata hivyo, mara baada ya kuwasili jana alasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam Mbunge huyo wa Kyela (CCM), hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari na badala yake alitoa ujumbe wake huo kupitia kwa Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa ambaye pia ni msemaji wa familia ya Dk Mwakyembe.

Mwambalaswa alisema Dk. Mwakyembe ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi tangu mwaka jana, amerejea akiwa na siha njema na kuongeza kuwa, Jumatatu atakuwa ofisini kwake wizara ya Ujenzi. Read more….

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO